o-level kurudishwa kwenye shule zilizokuwa na a-level tupu

o-level kurudishwa kwenye shule zilizokuwa na a-level tupu

Mpigamsuli

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2012
Posts
3,885
Reaction score
582
Wizara ya elimu imesema kwamba inarudisha madarasa ya o-level kwenye shule zilizokuwa na a-level tupu lengo ni kuwapa nafasi watoto wa darasa la saba ambao wanaufaulu wa kati na ambao wamekosa nafasi ya kwenda kwenye shule za vipaji maalumu kupata nafasi katika hizo shule ,hii itaongeza /itatoa nafasi kwa watoto hao kupata muda wa kutosha wa kujisomea
 
Hili wazo la serikali kurudisha o'level kwenye shule za advance tupu,naliunga mkono....shout out to Shukuru Kawambwa & Mulugo....

Mara nyingi ukiwela o'level kwenye shule ya advance,ufaulu unakuwa ni mzuri..vijana wanajifunza mengi kutoka kwa kaka zao...!!
 
waliwaza nini kuondoa olevel katika shule za advance, nnahisi litakuwa limechangia kuporomoka kwa elimu yetu Tanzania pia. ni safi sana, linawapa wanafunzi nafasi na mwamko zaidi wa kusoma!
 
Wizara ya elimu wanapewaga mawaziri misukule, na ndo maana huyu anapamnga hivi akija kichaa mwingine anapangua na anapanga vile.....!!hivi vitendo vinarudisha elimu Nyuma Huu mfumo ndo mzuri na ulikuwepo sijui nani akauparaganisha?

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Wizara ya elimu imesema kwamba inarudisha madarasa ya o-level kwenye shule zilizokuwa na a-level tupu lengo ni kuwapa nafasi watoto wa darasa la saba ambao wanaufaulu wa kati na ambao wamekosa nafasi ya kwenda kwenye shule za vipaji maalumu kupata nafasi katika hizo shule ,hii itaongeza /itatoa nafasi kwa watoto hao kupata muda wa kutosha wa kujisomea
Itaongeza kwa namna gani? Muda huo unatokana na uwepo wa a-level?
 
Double standard ya mfumo wa elimu kwenye nchi moja ni hatari sana mara masomo ya biashara yafutwe mara yarudishwe mara shule zenye Alevel Olevel waondolewe mara warudishwe ilimradi kila mtu anafanya anachotaka kwanini kusiwe na mfumo mmoja usio badilika badilika kama sheria ya Wamedi na Waajemi.
 
madogo wataopelekwa milambo watakoma kufanya usafi na kuchota maji makokola mpaka wawe manunda
 
hahaaa nakumbuka olevel form five wakija tulikuwa tunawaita njuka wa kiangaz/nyoya wa kiangaz/form one wa kiangaz..

sasa vipi kuhusu wale wenye division iv.26 ambao walisema watachukuliwa form v mbona kimya? Kulikoni? Maana mulugo aliahidi sasa mbona kimya... Wapo tu wanasubiri jibu la mulugo.... Na je kwa nini wasipewe nafasi ya kurisiti mwaka huu basi mbona kimya maana wengine hawakujisajili necta wapo njia panda
 
Mbona a level zipo wazi si wawachukue hao jamani binafsi ni wazo zuri maana ualimu hawajachaguliwa, kilimo hawachaguliwa basi wenye uwezo wapewe nafasi ya kuendelea kidato cha tano jamani... Wapi mulugo wapi shukuru kawambwa... Saidia janga hili litaangamia
 
Halafu hivi ule utaratibu kwamba ukirisiti matokeo yako ya awali yanafutwa bado upo kweli au maneno yasiyo kweli ya watu? Na je ukipata credit unaweza kufanya mtihani kama private candidate? Jamani mtuelimishe tusiojua
 
wait! wanaojua wanakuja
 
Wizara ya elimu imesema kwamba inarudisha madarasa ya o-level kwenye shule zilizokuwa na a-level tupu lengo ni kuwapa nafasi watoto wa darasa la saba ambao wanaufaulu wa kati na ambao wamekosa nafasi ya kwenda kwenye shule za vipaji maalumu kupata nafasi katika hizo shule ,hii itaongeza /itatoa nafasi kwa watoto hao kupata muda wa kutosha wa kujisomea

Huo mda utaongezekaje? hakuna jipya hapa ktk wizara ya elimu kila mtu anakuja na lake na ndomaana mfumo wetu wa elimu ni mbovu kutokana na wizara kuongozwa na vichwa maji.
 
Back
Top Bottom