Obad: Msikubali kusaliti mapambano ya kudai haki kivyovyote vile

Obad: Msikubali kusaliti mapambano ya kudai haki kivyovyote vile

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,040
Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Victoria, Zakaria Obad amewataka viongozi wa chama hicho, viongozi wa dini na wananchi kwa ujumla kutokubali kudanganyika na kusaliti mapambano ya kudai haki nchini.

Akizungumza na JAMBO TV siku ya Jumatano, Obad amedai siku za hivi karibuni baadhi ya viongozi wa chama hicho na viongozi wa dini wamekuwa wakishawishiwa kusaliti harakati za chama hicho za kudai haki kupitia kauli mbiu yao ya 'No Reforms No Election' akiwataka kuendelea na msimamo huo wa kudai haki.

Soma pia: Katibu CHADEMA kanda ya Victoria Zakaria Obad: Tumemaliza kutoa elimu sasa tufikirie tunasitishaje Uchaguzi


​

"Hadi sasa tunazo taarifa pamoja na kwamba mmefuatwa na kurubuniwa na kutapeliwa lakini mmekataa na kuendelea kusimama katika haki, tunawaomba sana Watanzania muendelee na msimamo huo, msikubali kamwe kusaliti mapambano ya kupigania haki, wapo ndugu na jamaa tumewapoteza kwa sababu ya kupigania haki," amesema Obad.​

 
 
Back
Top Bottom