Obama and his entire family are in Tanzania right now

OBAMA ATUA NCHINI KIMYA KIMYA

Na MWANDISHI WETU – KILIMANJARO

RAIS Mstaafu wa Marekani, Barack Obama, amewasili nchini kimya kimya akiwa na familia yake.

Hii ni mara ya pili kwa Obama kuja nchini, ambapo mara ya kwanza ilikuwa Julai 2013, wakati kiongozi huyo akiwa bado madarakani.

Ziara yake hiyo ya kikazi ilikuwa ni sehemu ya kukamilisha ratiba yake ya mwisho ya ziara barani Afrika wakati akiwa Rais.

Tofauti na ziara yake ya awali ambapo alikuja na ndege ya Air Force One akiwa na msafara unaolindwa na kila aina ya teknolojia, safari hii alikuja na familia yake lengo likielezwa kuwa ni kwa ajili ya kupumzika.

Chanzo cha uhakika kililiambia MTANZANIA kuwa Obama alitua nchini kimya kimya ambapo aliwasili Jumapili ya Julai 8, mwaka huu na kushukia katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) na kufanya mazungumzo na kiongozi mmoja mwandamizi wa Serikali katika eneo maalumu ambalo lilitengwa mjini Moshi.

Baada ya mazungumzo na kiongozi huyo wa Serikali yaliyodumu kwa takribani dakika 40, Obama alirejea KIA akiwa kwenye gari maalumu na kupanda ndege ndogo maalumu na kwenda kupumzika Mbuga ya Serengeti.

“Alipanda ndege ndogo akaenda Serengeti ambapo amefikia Singita Grumeti,” kilisema chanzo chetu.

Pamoja na hali hiyo inaelezwa kuwa Rais huyo Mstaafu wa Marekani, atakuwa hapa nchini kwa mapumziko ya wiki moja pamoja na familia yake.

Akiwa ndani ya Mbuga ya Serengeti atajionea utajiri mkubwa wa maliasili uliopo nchini pamoja na vivutio vyake ikiwamo wanyama.

Katika ziara yake ya mwaka 2013, Obama aliisifu Tanzania na kusema ni kama nyumbani kwake, kutokana na historia yake.

Alisema uhusiano uliopo kati yake na Tanzania, umewafanya baadhi ya wanafamilia wake kuwa na uhusiano wa kuitembelea Tanzania kwa shughuli mbalimbali

OBAMA ATUA NCHINI KIMYA KIMYA
 
Clouds ni media kubwa hapa Tanzania hawawezi kutoa habari ya uongo, kwanza wangelipa faini kwa sababu wametoa taarifa ambayo haijathibitishwa

Hao Clouds wameandika hapo kwa hio Tweet kwamba source yao ni 'mtandaoni'.
In short watoa hio habari hapa JF.
 
Hii habari yote ya Obama kuja Tanzania ilianzia papa hapa Jamii Forums.
Clouds wakichukua hio habari bila kudhibitisha wao wenyewe, na kufuatwa na media zingine.

So far hakuna any independent verification.
Therefore, treat it as fake news.
 
Hii habari yote ya Obama kuja Tanzania ilianzia papa hapa Jamii Forums.
Clouds wakichukua hio habari bila kudhibitisha wao wenyewe, na kufuatwa na media zingine.

So far hakuna any independent verification.
Therefore, treat it as fake news.
Soma hapo juu kwa Mwanzi1, hilo ni gazeti pia limetoa hiyo habari
 
Soma hapo juu kwa Mwanzi1, hilo ni gazeti pia limetoa hiyo habari

As I said, hii maneno yote ilianza hapa JF.
Clouds wakachukua uhondo bile kudhibitisha.
Kisha majigazeti mengine ambayo kila mtu anajua ni gutter newspapers.

Nitaamini haya maneno wakati picha zitatoka, au pale Obama atatua Nairobi kutoka Tanzania.
Kumbuka Obama anakuja Kenya Monday July 16.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…