Gaddafi alikuwa Dictator muovu aliyetumia pesa za mafuta kujinufaisha, kununua marafiki na kujichimbia madarakani.
Madikteta wote huwa wanaharibu kabisa taasisi na mifumo ya nchi kiasi cha kufikia kuwa wao ni dola na dola ni wao. Kwa sababu hiyo, wanapoondolewa madarakani kwa njia yoyote ile huwa wanaacha ombwe kubwa ambalo hujazwa na watu wasiojua chochote kuhusu uongozi na matokeo yake ni machafuko na ghasia kama unazozishuhudia Libya leo. Hicho pia ndicho kilichoipata Somalia ya Siad Bare baada ya utawala wake kuanguka, Nigeri, Congo na sehemu nyingine nyingi hivyo hivyo pia.