Ni Huduma gani za jamii ambazo ni mfano wa kuigwa? Elimu hamna kitu, Afya ndo usiseme, Mawasiliano mabovu, maji vijijini, yaani unajua hawa wakubwa wanapelekewa maendeleo kwenye karatasi lakini ki uhalisia hali ni mbaya. Ngoja hao jamaa waje kujifunza watapigwa changa lamcho tu. Unacheza na wabongo...................
Unaongea nini wewe?
1) Elimu wakati wa JMK, over 2000 secondary schools, haijatokea kwa rais yeyote aliopita, hata ukichanganya wooooooote na shule walizojenga kwa awamu zoooooooooooote, hawajafikia shule alizojenga JMK kwa muda mfupi.
Vyuo vikuu, zaidi ya 11, na vingine nane vipo njiani, kwa kipindi kifupi cha JMK. Kimoja kimevunja record ya dunia, toka kitangazwe mpaka kijengwe, mpaka kianze kuchukuwa wanafunzi, less than 2 years, si kingine bali ni UDOM. Hakuna ilipowahi kutokea namna hii na kwa muda huo.
2) Hospitali, uliza uambiwe, Huduma zinahamia hospital za wilaya, nenda hospital ya wilaya yako ukaone, hivyo ndivyo ilivyokuwa miaka minne nyuma? na sasa mkakati wa kujenga vituo vya afya kila kata umeanza, hayo huyajuwi? au huyaoni? Ni juzi tu, nilikuwa Aga Khan Hospital (Dar) kwa shughuli zangu, viongozi wa hiyo hospital wanalalamika, wauguzi na madaktari wanaacha kazi wanaenda hospital za serikali, kwa sasa zinalipa kuliko private tena kama Aga Khan inayosifika kwa kulipa. Jee, hayo huyajuwi? au huyaoni? au huyasikii?
3) Maji, nenda katizame miradi ya maji iliyopo sasa hivi katika kila wilaya, utalia kwa furaha, haijawahi kutokea. Kila wilaya inatakiwa ihakikishe wananchi wanapata maji safi na ya kutosha na mihela ipo teletele kwa miradi ya maji. Jee huyaoni hayo? au huyasikii?
4) Mabarabara, Singida - Babati - Minjingu (ilipoishia lami ya kiutoka Arusha) inajengwa tena kwa spidi ya hali ya juu. Dodoma - Babati hali kadhalika. Mkata - Handeni - Korogwe. Tayari imeanza juzi, nilikuwa huko. Na mengine kibao.
5) Mawasiliano ya simu, hii leo Tanzania mpaka vijijini unakula mtandao, wa simu na wa internet. Mimi ni shahidi wa hili, nna ki E61 changu, aaah, sijakosa mawasiliano, na nnasafiri karibu Tanzania nzima. Jee huyaoni hayo? Huyasikii?
Wengine huwa tunatazama wapi sijui, maendeleo hatuyaoni, wamerekani wanayaona sisi tupo hapa ndio tusiyaone? labda hatutaki kutazama.
6) Police Force, kwa sisi tunaesafiri sana, tunaona mabadiliko kutoka hata kwa ma trafiki waliopo barabarani. Sasa trafiki akikusimamisha anaanza kukusalimia, kwa sisi tunaamkiwa, tunaulizwa habari za safari, tunaambiwa samahani kwa kukuchelewesha tunataka kuhakikisha usalama wako na raia wengine tunaomba tukaguwe gari yako. Si mabadiliko hayo, wakati wa Nkapa polisi hawa walikuwa kama mbogo, hutaki hata kuongea nao. Sasa unaona raha wanavyoonyesha kujali.
Ama kweli asiyeona haambiwi tazama.