OBD 2 DIAGNOSTIC MACHINE

OBD 2 DIAGNOSTIC MACHINE

Brainze11

Senior Member
Joined
Sep 2, 2012
Posts
173
Reaction score
56
Inapima fault upande wa engine tu,inasoma fault code na kufuta, pia show live data stream. Ina support magari yanayotumia obd2 kuanzia 1996 hadi sasa. Inaweza kutumiwa na mafundi au mtu binafsi mwenye gar kwan ni rahisi kutumia.
Bei: 250,000
0714704097
79a8028c1a203f17f182dad7954144b6.jpg
7d1dc80577a6195fd4b4e9533c634a29.jpg

b8e93944150f76414d88ede7ade3b0ed.jpg
 
Mkuu saa nyingine mheshimu biashara za watu hata kama inauzwa iyo bei ujue kuna charges nyingine.

Kuna kusafirisha maushuru bado mleta mada analipia frame umeme na bando la kuandika humu kuna conviniences mbali mbali kama kusubiri mzigo etc

so kama anauza bei hiyo ujue kuna vitu viko calculated sio unajifanya unajua sna
 
Utandawazi raha, taja charges zako zote tujue imekuaje kutoka dola 35( 78,000/=) had dola 111.(250,000/) exchange rate 2250/dola. Kwa utandawazi huu kaka hakuna siri na ndo mana mnalalamika biashara ngumu kumbe mnataka faida kuubwa, utakuta bidhaa yenyewe ni used tena Internationa free shipping, kwa kifupi ndo biashara ishaingia mdudu
 
Mkuu saa nyingine mheshimu biashara za watu hata kama inauzwa iyo bei ujue kuna charges nyingine.

Kuna kusafirisha maushuru bado mleta mada analipia frame umeme na bando la kuandika humu kuna conviniences mbali mbali kama kusubiri mzigo etc

so kama anauza bei hiyo ujue kuna vitu viko calculated sio unajifanya unajua sna
Naheshimu sana biashara za watu na napenda mtu afanye "informed decision" anapotaka kufanya uamuzi wa kununua kitu au kutokununua. Soko huru ni wakati unapopata nafasi ya kulinganisha bei ya bidhaa. Anayeweza kuagiza nje aagize asiyeweza anunue kwa jamaa. Simple. Hapa JF tunasaidiana na sio kukomoana. Hiyo la kujifanya najua sana umeongea wewe.
 
ya kwangu nilinunua dola 28 +free shipping. matumizi yake zaidi kwangu huwa ni kuangalia engine performance wakati ikiwa idle kwani hunisaidia sana kujua iwapo oil au air cleaner vimechoka. Ninabadilisha oil mwenyewe na huwa sifuati idadi ya km bali nafuata engine performance. Kuna wakati naweza kubadilisha kwa miezi miwili tu na kuna wakati naweza kusubiri hadi miezi mitano kulingana na data ninazopata kutoka kwenye hii scanner. Iwapo una vifaa vya kutosha kwenye garage yako na wewe ni DIY kwenye magari yako, ni vizuri sana kuwa nayo.
 
Back
Top Bottom