Obrey Chirwa nikiumbe msumbufu uwanjani eeh au macho yangu?

MUTTAZ

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2016
Posts
296
Reaction score
237

Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa Chola amesema kwamba iwapo atapangwa katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya mahasimu, Simba Oktoba 1, mwaka huu atajenga heshima.

Akizungumza na Bin Zubeiry Sports Chirwa amesema kwamba amekuwa akijifua kwa bidii ili kumshawishi kocha Hans can der Pluijm ampe nafasi Oktoba 1.
“Najua bado sijawafurahisha mashabiki wa timu yangu (Yanga). Na ninajua nina deni. Lakini nawaomba watulie, mimi ninalifanyia kazi hilo,”amesema Chirwa aliyesajiliwa Julai mwaka huu kutoka Platinum FC ya Zimbabwe.

Chirwa ambaye hadi sasa amecheza mechi sita za mashindano yote Yanga bila kufunga bao hata moja, amesema kwamba anataka kucheza vizuri kuisaidia Yanga kushinda ili ajenge heshima yake.

“Mimi kufunga itakuwa kizuri, lakini nataka zaidi kucheza vizuri kuisaidia timu kushinda, yeyote atakayefunga ni sawa kwa faida ya timu,”amesema mchezaji huyo wa Zambia.

Chirwa bado hajazikonga nyoyo za mashabiki wa Yanga tangu amesajiliwa Julai kutokana na kutoonyesha kiwango kizuri na kukosa mabao ya wazi, ingawa anaonekana ni mchezaji mzuri.

Baadhi ya mashabiki wa Yanga wanaonekana kumkatia tamaa, lakini wengine nafsi zao zimeridhia kumpa muda kwa sababu wanaamini ni mchezaji mzuri.
 
Kwamba macho yako yamefanyaje
 
Ana Goli 5 katika mechi kama 4 hivi alizocheza katika ligi
 
Hakika Chirwa ameuwasha moto, Tambwe kama kawaida yake anaelekea kwenye njia sahihi ya kuchukua kiatu chake cha dhahabu.
 
Huu moto si wa mchezo huyu Chirwa alisema akianza kuwasha moto unakuwa unstoperble
 
Huu moto si wa mchezo huyu Chirwa alisema akianza kuwasha moto unakuwa unstoperble
Kuna yule wa upande wa pili wakati anasaini kandarasi aliombwa akatwe 1M akitoka uwanjani bila kufunga tunaomba mrejesho hadi sasa amekatwa kiasi gani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…