Observation: Maadili ya vijana yameshuka baada ya Jando na Unyago kuondoka ?

Observation: Maadili ya vijana yameshuka baada ya Jando na Unyago kuondoka ?

funaku

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2011
Posts
39,468
Reaction score
31,952
Hii ni observation yangu.

Baada ya Utandawazi kubomoa mfumo huu muhimu wa jamii yetu kwa kisingizio cha uasherati na ukeketaji sasa ndio tunaanza kuona matokeo yake halisi.

Vijana balehe wanaingia ukubwani bila kupata dose muhimu ya mabadikiko ya kimaumbile,jinsi ya kuishi na mwenza ,jinsi ya kuheshimu wenzao wa rika moja, jinsi ya wakubwa zao na jinsi ya kuja kutunza wadogo zao.
Badala yake vijana wanajifunza kuoitia tiktok na mbaya zaidi wanajifunza kutoka wanaharakati wenye background chafu.

Mungu atusaidie na awajaalie vijana wetu.

Lakini wizara husika ifikiri kukaa na Wazee wa Jadi,viongozi wenye kujiheshimu wa dini zote ili kuja na sessions/social events za kimaadili.

Wamasai kwa mbali wanaendelea kumantain.

Wazaramo wanapigwa vita sana eti vigodoro n.k.

Shime wanajamii tuamke na kuwasaidia vijana.
 
Wapeni kwanza vijana ajira za maana
 
Jando na unyago ilileta ujamaa, ila kutokana na mifumo ya kidunia kubadilika na kuwa kwenye ubepari, imekuwa kila kijana anapambana atoke vipi; hali inayopelekea maadili kuporomoka.​
 
These were the times long foretold.

This generation shall not pass...

Our redemption is nigh! !
 
Ajira za maana zimetoka sana aibu ni kwamba hata wenye ajira za maana kwa sasa hawana maadili
Toka hapa na maadili uchwara, wizi wa kura na ufisadi ndio uharibifu wa maadili zaidi wa kushughulika nao.
 
Hata hao wa zamani hawakuwa na maadili. Ndo waasisi wa ufisadi, katiba mbovu na madhambi mengine kibao yanayogharimu nchi hadi leo.
 
Yaani jando/unyago ndio vilete tumaini kwa taifa? Hao wanaitwa viongozi wamekulia karne ya 20 kukiwa na jando/unyago, ila madhambi wanayoyafanya hata shetani anashangaa walikotoa huo ujasiri.

Tunadai mifumo sawia katika nchi, misingi imara ya vyombo vya maamuzi ya kitaifa, familia bora, n.k

Mambo ya jando/unyago ni uduni wa fikra
 
Hii ni observation yangu.

Baada ya Utandawazi kubomoa mfumo huu muhimu wa jamii yetu kwa kisingizio cha uasherati na ukeketaji sasa ndio tunaanza kuona matokeo yake halisi.

Vijana balehe wanaingia ukubwani bila kupata dose muhimu ya mabadikiko ya kimaumbile,jinsi ya kuishi na mwenza ,jinsi ya kuheshimu wenzao wa rika moja, jinsi ya wakubwa zao na jinsi ya kuja kutunza wadogo zao.
Badala yake vijana wanajifunza kuoitia tiktok na mbaya zaidi wanajifunza kutoka wanaharakati wenye background chafu.

Mungu atusaidie na awajaalie vijana wetu.

Lakini wizara husika ifikiri kukaa na Wazee wa Jadi,viongozi wenye kujiheshimu wa dini zote ili kuja na sessions/social events za kimaadili.

Wamasai kwa mbali wanaendelea kumantain.

Wazaramo wanapigwa vita sana eti vigodoro n.k.

Shime wanajamii tuamke na kuwasaidia vijana.
Msingi mkubwa wa maadili kwa vijana ni malezi ya wazazi wenyewe.Jando na unyago vinasaidia lakini ni madarasa ya muda mfupi.siku hz ni nadra sana mzazi kumchapa mtoto kwa makoa afanyayo eti malezi ya zamani.Watoto wanaiga maisha ya wazazi wao nyimbani.je maisha ya bb na mm nyumbani yanatoa fundisho kwa watoto?baba arudi saa 6 usk na mama kwa sababu ya stress ananglia sinema zetu masaa12.unategemea nini kwa watoto
 
Back
Top Bottom