OC CID asema Godbless Lema hastahili kuota ndoto

OC CID asema Godbless Lema hastahili kuota ndoto

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
14,242
Reaction score
34,903
MKUU wa upelelezi wilaya ya Arusha(OC-CID), Damas Masawe (44) amesema wazee pekee ndio wanaotakiwa kuota ndoto hivyo Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema hakustahili kuota ndoto dhidi ya Rais John Magufuli kwa kuwa bado ni kijana.

Ameyasema hayo leo mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Arusha ,Devotha Msofe wakati akitoa ushahidi wake kwenye kesi ya uchochezi namba 440/2016 inayomkabili Lema anayedaiwa kumdhalilisha Rais Magufuli.

Ameieleza mahakama kuwa kwa mujibu wa kitabu cha kitakatifu cha biblia imeandikwa wazee pekee ndio wataota ndoto hivyo kwa kuwa Lema hajafikisha umri wa miaka 60 hatakiwi kuota ndoto bali wazee wanaotakiwa, wapumzike ,watafakari na kuota ndoto.

Hata hivyo shahidi huyo alieleza mahakama hiyo kuwa ingawa yeye sio mtaalamu wa masuala ya imani lakini anaamini kuota ndoto sio kosa ila kosa ni kuadithia ndoto .

“Kuota ndoto sio kosa lakini kuadithia ndoto yako ni kosa hayo maneno laiti ningekutana naye uchagani kama kaka yake angeniambia wala nisingekuwa na shida lakini aliyatolea mkutanoni," alieleza Massawe.

NILIMTOLEA LEMA BASTOLA

Shahidi huyo ameieleza mahakama kuwa alilazimika kumtolea bastola mbunge Lema katika eneo la kambi ya Fisi juni 22, mwaka jana kwani alikuwa anajaribu kutoroka.

Massawe alida kwenye eneo hilo Lema alikuwa akihutubia mkutano wa hadhara huku akisisitiza hana ugomvi na Lema kwa kuwa hata watoto wa mbunge huyo wanampenda sana.

Awali ,Massawe akiongozwa na wakili wa serikali,Agnes Hyera kutoa ushahidi wake alidai kuwa kwenye mkutano huo wa Lema kulikuwa na watu 200.

Alidai kitendo cha Lema kumwita Rais Magufuli ana kiburi na kumtabiria kifo ni kuamsha chuki kwa wananchi waliomchagua na hakupendezwa na maneno hayo na hivyo aliamua kumchukulia hatua kwani kwa wakati huo alikuwa akikaimu nafasi ya mkuu wa polisi wilaya ya Arusha.(OCD).

Shauri hilo linalovuta hisia za wengi limeahirishwa mpaka Januari 22,mwakani litakaposikilizwa siku tatu mfululizo mpaka januari 24 ambapo upande wa mashtaka unatarajia kuendelea kuleta mashahidi wengine.
 
Huyo Oc CID mbona ata mwanangu Wa miaka 3 anamzidi kwa kuongea vitu vya maana? anaweza kweli kupelekwa kutoa ushahidi kwenye independent institution?
Wanahitaji kuombewa kuanzia Mkuu wa nchi,hawastaili kulaumiwa bali kuhurumiwa,mambo yamewashinda ni frustration tu.Yeye mwenyew anajua mambo magumu,ameivuruga nchi kwa kua mipango mibovu isiyoshirikishi kana kwamba anaongoza familia kumbe nchi ya watu.
 
1.Hatutakiwi kusema Vyuma vimekaza.
2. Hatutakiwi kuota ndoto before 60 yrs.

Mpk huu utawala ukome tutakua tushapangiwa mpk bao za kupiga kwa wake zetu.
Na pia kuanzia mwezi ujao magazeti ya kusoma mmeambiwa ni UHURU na MZALENDO,,
NA Ukikutwa au kusikika unalalamika hali ngumu unaenda jela miezi sita" [HASHTAG]#TwaFA[/HASHTAG]
 
Iwapo watanzania kiendelea kusali na kuomba basi Mola atasikia vilio
 
Hivi ni vituko vys karne au vya kufunga mwaka 2017. Yaani kuota ndoto ni kwa wazee tu!!!!

Hivi shahid alijiandaa kabla ya kutoa haya maneno????
 
Hivi ni vituko vys karne au vya kufunga mwaka 2017. Yaani kuota ndoto ni kwa wazee tu!!!!

Hivi shahid alijiandaa kabla ya kutoa haya maneno????
 
Wanahitaji kuombewa kuanzia Mkuu wa nchi,hawastaili kulaumiwa bali kuhurumiwa,mambo yamewashinda ni frustration tu.Yeye mwenyew anajua mambo magumu,ameivuruga nchi kwa kua mipango mibovu isiyoshirikishi kana kwamba anaongoza familia kumbe nchi ya watu.
Nyie hamuombi invlavyotakiwa. Mnayatibua mapepo. Kisha mnayaacha yanapata kisirani.
 
Back
Top Bottom