OC - CID Mafwele ni nani? Kwanini haguswi na uhamisho wa Polisi nchini?

OC - CID Mafwele ni nani? Kwanini haguswi na uhamisho wa Polisi nchini?

buswelu moja

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2014
Posts
226
Reaction score
180
HIVI OC-CID MAFWELE NI NANI? WENYE DATA ZIMWAGENI HAPA

Kwa mtu ambaye ni mkazi wa jiji la Arusha na viunga vyake nadhani atakuwa anamjua vizuri mkuu wa upelelezi wilaya ya Arusha,OC-CID Faustine Mafwele.

Kiongozi huyu wa jeshi la polisi amekuwa akilalamikiwa kwa kiasi kikubwa kwa kukandamiza haki za raia kwa mfano kuwatia ndani baadhi ya watu ambao ana ugomvi nao bila sababu za msingi.

Mafwele amekuwa akilalamikiwa kwamba anazuia watuhumiwa wasipewe dhamana kwa jeuri yake hata kama dhamana ni haki ya mshtakiwa.

Analalamikiwa kwa tuhuma za rushwa ambazo amekuwa akiomba kwa baadhi ya watuhumiwa na pindi wanapokataa kumpa huwabambikia kesi mbalimbali.

Baadhi ya askari wanamtaja Mafwele kama kiongozi katili, jeuri mwenye majidai ambaye amejijengea mtandao wa askari wake ambao humpelekea kitu kidogo ofisini kwake ili awalinde pindi wanapokiuka sheria za jeshi la polisi.

Kuna taarifa kwamba hata RPC wa mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas anamwogopa Mafwele kwa kuwa ni mtu ambaye amejenga mtandao mpana katika makao makuu ya jeshi hilo jijini Dar na katika kuthibitisha hilo majuzi yalipofanywa mabadiliko ndani ya jeshi hilo nchi nzima Mafwele hakuguswa; mnajua kwanini? Swali hilo IGP Mangu atalijibu hapa.

Kama mnakumbuka mwaka juzi Mafwele alipigwa risasi ya bega la kulia na majambazi na tetesi zinasema kuwa aliwazunguka katika mgao wa fedha walizopora katika hoteli ya Kibo Palace ambayo ni mali ya tajiri Laswai.

Mafwele amejenga nyumba ya kifahari mkoani Mwanza wilayani Ilemela na nje ya nyumba hiyo eneo la parking kuna magari zaidi ya matano ya kifahari yamepaki nje hayatumiki huyu kigogo ana pesa kiasi gani?

Amedumu mkoani Arusha kwa muda wa zaidi ya miaka mitano bila kuhamishwa na kila uhamisho ukifika yeye haguswi je kuna nini hapa ndugu wadau embu tuulizane au ndiyo mtindo wa kulindana?

Kuna baadhi ya mahabusu hadi sasa wanasota jela la Kisongo na inasemekana baadhi yao amewabambikia kesi baada ya kushindwa kumpa rushwa ya kati ya sh, 4 hadi 5 milioni, na ukifika ofisini kwake kuna mafaili kibao ya watuhumiwa ambayo, ili kuyafuta anataka pesa.

Tunamwomba IGP Mangu amchunguze huyu kigogo wa jeshi la polisi Arusha kwani malalamiko yamekuwa mengi. Lakini naomba tujadili huyu Mafwele ni nani na alitokea wapi hadi kuukwaa u OC CID?

Wenye data zimwageni hapa.

Source: Mdau wa habari Arusha.
 
Hapo kuna mawili! Ukute yeye Ndio kiboko ya mitandao ya majambazi ya Arusha ; Sasa wanatengeneza fitna atolewe jeshi lipoteze dira na majambazi kujipanga na kuanza kusumbua!! Au hizo tuhuma ni za kweli!!

Sawa kabisa, na swala siyo kumhamisha kama ana makosa , bali makosa yake yachunguzwe kama ni kweli au vipi halafu hatua za kinidham zichukuliwe.
 
Hapo kuna mawili! Ukute yeye Ndio kiboko ya mitandao ya majambazi ya Arusha ; Sasa wanatengeneza fitna atolewe jeshi lipoteze dira na majambazi kujipanga na kuanza kusumbua!! Au hizo tuhuma ni za kweli!!

KWA KUWA UMESEMA MAFWELE NI KIBOKO YA MAJAMBAZI, BASI Ahamishiwe RORYA Huko TARIME ILI AKAPAMBANE NA WA HUKO, AU Apelekwe PEMBA YA ZANZIBAR AKAPAMBANE NA WA HUKO. ARUSHA TULETEWE MWINGINE. Pia Si Vibaya Akahamishiwa Wilayani Kwako.
 
Huyu jamaa ni huyo huyo ninayemfahamu alisoma Geita Sec. Miaka ya 80' katikati? Mafwele ni Mkara, alikuwa katibu wa shule na alikuwa katili sana kiasi vijana wa kidato cha kwanza tulikuwa tunamwogopa utafikri naye ni headmaster! Kama ndo yeye basi kumbe watu huwa hatubadiliki!
 
KWA KUWA UMESEMA MAFWELE NI KIBOKO YA MAJAMBAZI, BASI Ahamishiwe RoLYA Huko TARIME ILI AKAPAMBANE NA WA HUKO, AU Apelekwe PEMBA YA ZANZIBAR AKAPAMBANE NA WA HUKO.ARUSHA TULETEWE MWINGINE. Pia Si Vibaya Akahamishiwa Wilayani Kwako.

Wakubwa wake wameona yeye ndo anaye faa kufanyia kazi hapo sasa iweje malalamiko ya mtu mmoja aonekane haifai?
 
Huyu jamaa ni huyo huyo ninayemfahamu alisoma Geita Sec. miaka ya 80' katikati? Mafwele ni Mkara, alikuwa katibu Wa shule na alikuwa katili sana kiasi vijana Wa kidato cha kwanza tulikuwa tunamwogopa utafikri naye ni headmaster! Kama ndo yeye basi kumbe watu huwa hatubadiliki!

Naam ndo yeye. Ananduguye Zabahu mafwele tulikuwa wote Tabora School, roho mbaya
 
Huyu jamaa ni huyo huyo ninayemfahamu alisoma Geita Sec. miaka ya 80' katikati? Mafwele ni Mkara, alikuwa katibu Wa shule na alikuwa katili sana kiasi vijana Wa kidato cha kwanza tulikuwa tunamwogopa utafikri naye ni headmaster! Kama ndo yeye basi kumbe watu huwa hatubadiliki!

Taarifa kama hizi Watanzania huwa wanazificha hadi mtu anakuwa rais. Huwa siamini kama watu waliosoma na Lowassa, Slaa, Lipumba,nk hawapo...
 
Back
Top Bottom