OCD inanitesa, sijui nifanyeje!

OCD inanitesa, sijui nifanyeje!

Forgotten

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2018
Posts
3,518
Reaction score
10,839
Habari wana-JF. Obsessive compulsive disorder ni ugonjwa unaonisumbua kwa miaka mingi. Kama ilivyo kwa wengi ni ngumu kujijua kuwa wana matatizo ya akili. Niliishi miaka mingi nikijiona wa tofauti ila niliamini ni jinsi nilivyo tu bila kujua nina tatizo linalowakumba watu wengi tu Duniani.

Nilijua kuhusu OCD kwa mara ya kwanza hapahapa JF kupitia uzi ulioelezea tatizo hilo. Nilichukulia poa kwa kudhani ni jambo la kawaida ila jinsi siku zinavyozidi kwenda maisha yangu yanakuwa ya tofauti na watu wanaonizunguka.

Hali ninazozipata ni:

1. Mysophobia / Germophobia - extreme fear of germs and contamination. Aisee hiki kitu kinanitesa vibaya mno. Nimekuwa ni mtu wa kunawa mikono pale nitakaposhika kitu chochote kile, siwezi kushika kitasa cha mlango kwa mkono mtupu aidha nitatumia karatasi au nikishika basi moja kwa moja ni kuchukua sabuni na kunawa mikono. Kitu kikianguka chini siokoti. Mtu akigusa chakula changu siwezi tena kula hicho chakula. Siwezi kumpa mtu mkono labda iwe ni lazima kufanya hivyo. Nikiwa nakula mkono wangu wa kulia ni maalumu kwa kazi hiyo tu na ikitokea nimeshika kitu chochote kwa bahati mbaya basi nitaacha kula na kwenda kunawa tena. Siwezi kutumia kitu chochote kwenye public toilet, kama ni ndoo nitatumia ya kwangu peke yangu.

Hali hii inanitesa na kufanya kuwa ngumu mimi kuchangamana na jamii na watu wanaonizunguka kwasababu ni ngumu watu kuelewa tatizo nililonalo.

2. False memory OCD - hapa ndiyo tatizo kubwa lilipo. Napata msongo wa mawazo kutokana na matukio yasiyo ya kweli yanayotengenezwa na ubongo wangu. Ninaweza kukaa ghafla tu nikapata mawazo kuwa kuna jambo baya limenitokea wakati uliopita na nitatumia masaa kulirudia hilo tukio kwa kila namna lilivyoweza kutokea nikijua fika siyo kweli mpaka pale nitakapopata ahueni au kuhisi hakuna kilichotokea. Kuna kipindi nilitumia siku 3 mfululizo nikiwa na mawazo tu, ni jambo linalonipotezea muda ila nashindwa kujizuia kabisa. Kwa watu ninaoishi nao huwa naweza kuwauliza maswali ili kupata uhakika wa tukio fulani kutokea na wakinipa majibu yasiyokamilika ndiyo mawazo yanazidi kabisa.

3. Real events OCD - hapa huwa napata mawazo mengi kuhusu mambo niliyowahi kufanya wakati uliopita. Vitendo hivyo huwa vinanipa mawazo nikijihisi nimekosea watu au nilifanya vitendo vya aibu. Matukio hayo huwa yanafanya najutia vitu nilivyowahi kufanya. Ni ngumu kukwepa hayo mawazo kwasababu yanajirudia kila muda ninapokuwa nimetulia.

Mawazo imekuwa ni sehemu ya maisha yangu.

3. Compulsive / repetitive behaviors - vitendo hivi vya kujirudia ndiyo zilikuwa dalili za mwanzo na kujigundua kuwa nina OCD. Mwanzo nilikuwa naona ni vitu vya kawaida tu. Kuosha mikono mara kwa mara, kuhakiki kuwa nimefunga mlango na kuhesabu: namba ninazozihesabu ni 1-7 au 1-10, bila kufanya hivyo nitakuwa na wasiwasi usioelezeka na hata nikihakiki bado ninakuwa na hofu na nashindwa kujizuia kupata hofu. Kuuliza maswali kuhusu matukio fulani ambayo hayajawahi kutokea ili tu nipate uhakika. Kukwepa maeneo yanayopeleka mimi kupata mawazo ya kitu fulani, mahali ninapoishi kuna njia sipiti japokuwa ndiyo shortcut ya kwenda dukani. Nikipita hiyo njia basi mawazo yataanza, sababu wala siyo ya msingi ila nashindwa kabisa kuzuia hilo.

OCD imepelekea maisha yangu ya kijamii kuwa magumu kwa kuogopa kufanya vitu kadhaa nikiogopa matukio mabaya kutokea. Mawazo ndiyo yametawala maisha yangu, nimekuwa mtu wa peke yangu peke yangu tu. Nashindwa hata kuwaeleza watu wangu wa karibu hali ninayopitia kwasababu nahisi hawatanielewa kwa kuona siyo tatizo.

Mbaya zaidi tatizo hili siyo rahisi kuondoka ni hali ambayo inanibidi niishi nayo. Ningependa kujua wale wanaopitia hali hii kipi kimewasaidia kupunguza hili tatizo.
 
Mbaya zaidi tatizo hili siyo rahisi kuondoka ni hali ambayo inanibidi niishi nayo.
Umejifunga hapa!

Katika kutoa ushauri client ndiye anakuwa na solution ya tatizo lake.

Kama utakubali kuwa unaweza kuchange fanya hivyo kwa kuchukua hatua Mara 1. Maisha ni kujifunza

Kama unaamini huwezi kubali kuishi vile ulivyo. Itafikia watu watakuelewa tu.
 
Unahitaji tiba haraka mno....

Kuna hatua mbili....

1)Psychotherapy....mazungumzo na mshauri tiba ambaye atakuandalia hatua tiba.

2)Madawa yaitwayo Antidepressants.....

Pole sana mkuu na kila la heri katika matibabu hayo ,amen[emoji120]

#DoNotDoHarm[emoji120]
 
Habari wana-JF. Obsessive compulsive disorder ni ugonjwa unaonisumbua kwa miaka mingi. Kama ilivyo kwa wengi ni ngumu kujijua kuwa wana matatizo ya akili...
Mgonjwa unasema tatizo si rahisi kuondoka?!!! [emoji15][emoji15][emoji15]

Huo ndio UGONJWA wenyewe....

Nimekueleza hapo juu nenda hospitali ukutane na Psychiatrist atakusaidia ila humu utakuwa unatafuta tiba ya mazungumzo(psychotherapy) ambayo si RASMI na hata kama utapewa majibu na wataalamu wa afya ya akili haitokuwa bora zaidi ya kukutana nao....

Kila la heri [emoji120]
 
Mimi nilikuwaga na tatizo la over thinking, na imagine vitu ambayo havipo au kitu nikiwaza natengeneza scenario kibao tatizo hili nililimaliza baada ya kupewa ushauri mdogo tuu kwamba nitafute hobby ninayo penda ninywe bia kidogo niwe na tabia ya kutoka usiku na kutembea maeneo tofauti tofauti na pia nilipewa recomendation ya kusoma vitabu vya napoleon hill haswa haswa outwiting the devil niliacha hiyo tabia na mpaka sasa naishi vizuri una bahati wewe huna aibu mimi kilifika mda naogopa kuonekana nikiwa na tembea naona watu wananiangalia au wananisema
 
Unahitaji tiba haraka mno....

Kuna hatua mbili....

1)Psychotherapy....mazungumzo na mshauri tiba ambaye atakuandalia hatua tiba.

2)Madawa yaitwayo Antidepressants.....

Pole sana mkuu na kila la heri katika matibabu hayo ,amen[emoji120]

#DoNotDoHarm[emoji120]
Asante kwa maoni. Nitaufanyia kazi ushauri wako.
 
Umejifunga hapa!

Katika kutoa ushauri client ndiye anakuwa na solution ya tatizo lake.

Kama utakubali kuwa unaweza kuchange fanya hivyo kwa kuchukua hatua Mara 1. Maisha ni kujifunza

Kama unaamini huwezi kubali kuishi vile ulivyo. Itafikia watu watakuelewa tu.
Nimeichukua hii. Asante kwa ushauri.
 
Habari wana-JF. Obsessive compulsive disorder ni ugonjwa unaonisumbua kwa miaka mingi. Kama ilivyo kwa wengi ni ngumu kujijua kuwa wana matatizo ya akili. Niliishi miaka mingi nikijiona wa tofauti ila niliamini ni jinsi nilivyo tu bila kujua nina tatizo linalowakumba watu wengi tu Duniani.

Nilijua kuhusu OCD kwa mara ya kwanza hapahapa JF kupitia uzi ulioelezea tatizo hilo. Nilichukulia poa kwa kudhani ni jambo la kawaida ila jinsi siku zinavyozidi kwenda maisha yangu yanakuwa ya tofauti na watu wanaonizunguka.

Hali ninazozipata ni:

1. Mysophobia / Germophobia - extreme fear of germs and contamination. Aisee hiki kitu kinanitesa vibaya mno. Nimekuwa ni mtu wa kunawa mikono pale nitakaposhika kitu chochote kile, siwezi kushika kitasa cha mlango kwa mkono mtupu aidha nitatumia karatasi au nikishika basi moja kwa moja ni kuchukua sabuni na kunawa mikono. Kitu kikianguka chini siokoti. Mtu akigusa chakula changu siwezi tena kula hicho chakula. Siwezi kumpa mtu mkono labda iwe ni lazima kufanya hivyo. Nikiwa nakula mkono wangu wa kulia ni maalumu kwa kazi hiyo tu na ikitokea nimeshika kitu chochote kwa bahati mbaya basi nitaacha kula na kwenda kunawa tena. Siwezi kutumia kitu chochote kwenye public toilet, kama ni ndoo nitatumia ya kwangu peke yangu.

Hali hii inanitesa na kufanya kuwa ngumu mimi kuchangamana na jamii na watu wanaonizunguka kwasababu ni ngumu watu kuelewa tatizo nililonalo.

2. False memory OCD - hapa ndiyo tatizo kubwa lilipo. Napata msongo wa mawazo kutokana na matukio yasiyo ya kweli yanayotengenezwa na ubongo wangu. Ninaweza kukaa ghafla tu nikapata mawazo kuwa kuna jambo baya limenitokea wakati uliopita na nitatumia masaa kulirudia hilo tukio kwa kila namna lilivyoweza kutokea nikijua fika siyo kweli mpaka pale nitakapopata ahueni au kuhisi hakuna kilichotokea. Kuna kipindi nilitumia siku 3 mfululizo nikiwa na mawazo tu, ni jambo linalonipotezea muda ila nashindwa kujizuia kabisa. Kwa watu ninaoishi nao huwa naweza kuwauliza maswali ili kupata uhakika wa tukio fulani kutokea na wakinipa majibu yasiyokamilika ndiyo mawazo yanazidi kabisa.

3. Real events OCD - hapa huwa napata mawazo mengi kuhusu mambo niliyowahi kufanya wakati uliopita. Vitendo hivyo huwa vinanipa mawazo nikijihisi nimekosea watu au nilifanya vitendo vya aibu. Matukio hayo huwa yanafanya najutia vitu nilivyowahi kufanya. Ni ngumu kukwepa hayo mawazo kwasababu yanajirudia kila muda ninapokuwa nimetulia.

Mawazo imekuwa ni sehemu ya maisha yangu.

3. Compulsive / repetitive behaviors - vitendo hivi vya kujirudia ndiyo zilikuwa dalili za mwanzo na kujigundua kuwa nina OCD. Mwanzo nilikuwa naona ni vitu vya kawaida tu. Kuosha mikono mara kwa mara, kuhakiki kuwa nimefunga mlango na kuhesabu: namba ninazozihesabu ni 1-7 au 1-10, bila kufanya hivyo nitakuwa na wasiwasi usioelezeka na hata nikihakiki bado ninakuwa na hofu na nashindwa kujizuia kupata hofu. Kuuliza maswali kuhusu matukio fulani ambayo hayajawahi kutokea ili tu nipate uhakika. Kukwepa maeneo yanayopeleka mimi kupata mawazo ya kitu fulani, mahali ninapoishi kuna njia sipiti japokuwa ndiyo shortcut ya kwenda dukani. Nikipita hiyo njia basi mawazo yataanza, sababu wala siyo ya msingi ila nashindwa kabisa kuzuia hilo.

OCD imepelekea maisha yangu ya kijamii kuwa magumu kwa kuogopa kufanya vitu kadhaa nikiogopa matukio mabaya kutokea. Mawazo ndiyo yametawala maisha yangu, nimekuwa mtu wa peke yangu peke yangu tu. Nashindwa hata kuwaeleza watu wangu wa karibu hali ninayopitia kwasababu nahisi hawatanielewa kwa kuona siyo tatizo.

Mbaya zaidi tatizo hili siyo rahisi kuondoka ni hali ambayo inanibidi niishi nayo. Ningependa kujua wale wanaopitia hali hii kipi kimewasaidia kupunguza hili tatizo.

Kumbe mgonjwa wa akili ndio maana umekana imani ya Mungu. Tibu kwanza hii.
 
Unajifanya kuugua magonjwa ya kizungu eee ya kiswahili aaaaa,
Lugha ya Kiswahili haijitoshelezi ndiyo maana kuna maneno yametokana na utohozi.

Pia, hakuna mtu anayejifanya kuugua.
 
Daah noma sana umenikumbusha ndugu yangu mmoja aliwahi pata tatizo lile daaah..
Jamaa alikua akichukua udhu kwa ajili yakwenda msikitini kila akimaliza kwenye miguu ili aondoke anapata hofu kwamba hajatawadha kifupi anasahau kabisaa👈 daah jamaa alikua anakaa hapo kwenye bomba masaa.
Nihadi muweke msisitizo haswa kumwambia mbona unaludia ludia tena namuda unaenda?
Jamaa anajibu aisee nilikua nimesahau baadhi ya viungo kuweka maji ngoja nianze sasa upya.anaanza tena sasa.
 
Matajiri mna magonjwa ya ajabu ila yana majina mazuri hadi raha, eti OCD haaaa haaa haaa
 
Lugha ya Kiswahili haijitoshelezi ndiyo maana kuna maneno yametokana na utohozi.

Pia, hakuna mtu anayejifanya kuugua.

Hamna lolote nenda milembe hospitali huko wanatibu magonjwa ya akili
 
Habari wana-JF. Obsessive compulsive disorder ni ugonjwa unaonisumbua kwa miaka mingi. Kama ilivyo kwa wengi ni ngumu kujijua kuwa wana matatizo ya akili. Niliishi miaka mingi nikijiona wa tofauti ila niliamini ni jinsi nilivyo tu bila kujua nina tatizo linalowakumba watu wengi tu Duniani.

Nilijua kuhusu OCD kwa mara ya kwanza hapahapa JF kupitia uzi ulioelezea tatizo hilo. Nilichukulia poa kwa kudhani ni jambo la kawaida ila jinsi siku zinavyozidi kwenda maisha yangu yanakuwa ya tofauti na watu wanaonizunguka.

Hali ninazozipata ni:

1. Mysophobia / Germophobia - extreme fear of germs and contamination. Aisee hiki kitu kinanitesa vibaya mno. Nimekuwa ni mtu wa kunawa mikono pale nitakaposhika kitu chochote kile, siwezi kushika kitasa cha mlango kwa mkono mtupu aidha nitatumia karatasi au nikishika basi moja kwa moja ni kuchukua sabuni na kunawa mikono. Kitu kikianguka chini siokoti. Mtu akigusa chakula changu siwezi tena kula hicho chakula. Siwezi kumpa mtu mkono labda iwe ni lazima kufanya hivyo. Nikiwa nakula mkono wangu wa kulia ni maalumu kwa kazi hiyo tu na ikitokea nimeshika kitu chochote kwa bahati mbaya basi nitaacha kula na kwenda kunawa tena. Siwezi kutumia kitu chochote kwenye public toilet, kama ni ndoo nitatumia ya kwangu peke yangu.

Hali hii inanitesa na kufanya kuwa ngumu mimi kuchangamana na jamii na watu wanaonizunguka kwasababu ni ngumu watu kuelewa tatizo nililonalo.

2. False memory OCD - hapa ndiyo tatizo kubwa lilipo. Napata msongo wa mawazo kutokana na matukio yasiyo ya kweli yanayotengenezwa na ubongo wangu. Ninaweza kukaa ghafla tu nikapata mawazo kuwa kuna jambo baya limenitokea wakati uliopita na nitatumia masaa kulirudia hilo tukio kwa kila namna lilivyoweza kutokea nikijua fika siyo kweli mpaka pale nitakapopata ahueni au kuhisi hakuna kilichotokea. Kuna kipindi nilitumia siku 3 mfululizo nikiwa na mawazo tu, ni jambo linalonipotezea muda ila nashindwa kujizuia kabisa. Kwa watu ninaoishi nao huwa naweza kuwauliza maswali ili kupata uhakika wa tukio fulani kutokea na wakinipa majibu yasiyokamilika ndiyo mawazo yanazidi kabisa.

3. Real events OCD - hapa huwa napata mawazo mengi kuhusu mambo niliyowahi kufanya wakati uliopita. Vitendo hivyo huwa vinanipa mawazo nikijihisi nimekosea watu au nilifanya vitendo vya aibu. Matukio hayo huwa yanafanya najutia vitu nilivyowahi kufanya. Ni ngumu kukwepa hayo mawazo kwasababu yanajirudia kila muda ninapokuwa nimetulia.

Mawazo imekuwa ni sehemu ya maisha yangu.

3. Compulsive / repetitive behaviors - vitendo hivi vya kujirudia ndiyo zilikuwa dalili za mwanzo na kujigundua kuwa nina OCD. Mwanzo nilikuwa naona ni vitu vya kawaida tu. Kuosha mikono mara kwa mara, kuhakiki kuwa nimefunga mlango na kuhesabu: namba ninazozihesabu ni 1-7 au 1-10, bila kufanya hivyo nitakuwa na wasiwasi usioelezeka na hata nikihakiki bado ninakuwa na hofu na nashindwa kujizuia kupata hofu. Kuuliza maswali kuhusu matukio fulani ambayo hayajawahi kutokea ili tu nipate uhakika. Kukwepa maeneo yanayopeleka mimi kupata mawazo ya kitu fulani, mahali ninapoishi kuna njia sipiti japokuwa ndiyo shortcut ya kwenda dukani. Nikipita hiyo njia basi mawazo yataanza, sababu wala siyo ya msingi ila nashindwa kabisa kuzuia hilo.

OCD imepelekea maisha yangu ya kijamii kuwa magumu kwa kuogopa kufanya vitu kadhaa nikiogopa matukio mabaya kutokea. Mawazo ndiyo yametawala maisha yangu, nimekuwa mtu wa peke yangu peke yangu tu. Nashindwa hata kuwaeleza watu wangu wa karibu hali ninayopitia kwasababu nahisi hawatanielewa kwa kuona siyo tatizo.

Mbaya zaidi tatizo hili siyo rahisi kuondoka ni hali ambayo inanibidi niishi nayo. Ningependa kujua wale wanaopitia hali hii kipi kimewasaidia kupunguza hili tatizo.
Achana na hio tabia number moja ...sio ugonjwa ni upumbavu kufungua kitasa kwa kashika na karatasi au kutookota kitu yaan nikitabia cha kukera
 
Matajiri mna magonjwa ya ajabu ila yana majina mazuri hadi raha, eti OCD haaaa haaa haaa
Ocd ni ukichaa mkuu ni utindio wa ubongo ..mfano jamaa .kasema mtu akigusa chakula chake anakiacha sasa Mama n'tilie atampaje chakula bila kukigusa ,
Mara ubongo wake unatengeneza kumbukumbu za uwongo .asa hapo ukiwa karib yake afu ubongo ukamtengenezea kumbukumbu fake kua anakudai si shida hapo
 
Magonjwa mengine kwa Waafrika ni kujidekeza tu hayo ni magonjwa ya weupe.

Muafrika magonjwa yako ni malaria kifaduro kipindupindu na magonjwa mengine ya matumbo acha kulia lia kuiga visivyokuhusu,hata ushoga kwa Africa uliingia hivi hivi watu walipoona weupe wanaupigia debe kwamba ni tatizo la hormone weusi nao wakaunga trailer but weupe hao hao wangesema u$£nge ni ugonjwa wa akili Waafrika wasingeiga.
 
Habari wana-JF. Obsessive compulsive disorder ni ugonjwa unaonisumbua kwa miaka mingi. Kama ilivyo kwa wengi ni ngumu kujijua kuwa wana matatizo ya akili. Niliishi miaka mingi nikijiona wa tofauti ila niliamini ni jinsi nilivyo tu bila kujua nina tatizo linalowakumba watu wengi tu Duniani.

Nilijua kuhusu OCD kwa mara ya kwanza hapahapa JF kupitia uzi ulioelezea tatizo hilo. Nilichukulia poa kwa kudhani ni jambo la kawaida ila jinsi siku zinavyozidi kwenda maisha yangu yanakuwa ya tofauti na watu wanaonizunguka.

Hali ninazozipata ni:

1. Mysophobia / Germophobia - extreme fear of germs and contamination. Aisee hiki kitu kinanitesa vibaya mno. Nimekuwa ni mtu wa kunawa mikono pale nitakaposhika kitu chochote kile, siwezi kushika kitasa cha mlango kwa mkono mtupu aidha nitatumia karatasi au nikishika basi moja kwa moja ni kuchukua sabuni na kunawa mikono. Kitu kikianguka chini siokoti. Mtu akigusa chakula changu siwezi tena kula hicho chakula. Siwezi kumpa mtu mkono labda iwe ni lazima kufanya hivyo. Nikiwa nakula mkono wangu wa kulia ni maalumu kwa kazi hiyo tu na ikitokea nimeshika kitu chochote kwa bahati mbaya basi nitaacha kula na kwenda kunawa tena. Siwezi kutumia kitu chochote kwenye public toilet, kama ni ndoo nitatumia ya kwangu peke yangu.

Hali hii inanitesa na kufanya kuwa ngumu mimi kuchangamana na jamii na watu wanaonizunguka kwasababu ni ngumu watu kuelewa tatizo nililonalo.

2. False memory OCD - hapa ndiyo tatizo kubwa lilipo. Napata msongo wa mawazo kutokana na matukio yasiyo ya kweli yanayotengenezwa na ubongo wangu. Ninaweza kukaa ghafla tu nikapata mawazo kuwa kuna jambo baya limenitokea wakati uliopita na nitatumia masaa kulirudia hilo tukio kwa kila namna lilivyoweza kutokea nikijua fika siyo kweli mpaka pale nitakapopata ahueni au kuhisi hakuna kilichotokea. Kuna kipindi nilitumia siku 3 mfululizo nikiwa na mawazo tu, ni jambo linalonipotezea muda ila nashindwa kujizuia kabisa. Kwa watu ninaoishi nao huwa naweza kuwauliza maswali ili kupata uhakika wa tukio fulani kutokea na wakinipa majibu yasiyokamilika ndiyo mawazo yanazidi kabisa.

3. Real events OCD - hapa huwa napata mawazo mengi kuhusu mambo niliyowahi kufanya wakati uliopita. Vitendo hivyo huwa vinanipa mawazo nikijihisi nimekosea watu au nilifanya vitendo vya aibu. Matukio hayo huwa yanafanya najutia vitu nilivyowahi kufanya. Ni ngumu kukwepa hayo mawazo kwasababu yanajirudia kila muda ninapokuwa nimetulia.

Mawazo imekuwa ni sehemu ya maisha yangu.

3. Compulsive / repetitive behaviors - vitendo hivi vya kujirudia ndiyo zilikuwa dalili za mwanzo na kujigundua kuwa nina OCD. Mwanzo nilikuwa naona ni vitu vya kawaida tu. Kuosha mikono mara kwa mara, kuhakiki kuwa nimefunga mlango na kuhesabu: namba ninazozihesabu ni 1-7 au 1-10, bila kufanya hivyo nitakuwa na wasiwasi usioelezeka na hata nikihakiki bado ninakuwa na hofu na nashindwa kujizuia kupata hofu. Kuuliza maswali kuhusu matukio fulani ambayo hayajawahi kutokea ili tu nipate uhakika. Kukwepa maeneo yanayopeleka mimi kupata mawazo ya kitu fulani, mahali ninapoishi kuna njia sipiti japokuwa ndiyo shortcut ya kwenda dukani. Nikipita hiyo njia basi mawazo yataanza, sababu wala siyo ya msingi ila nashindwa kabisa kuzuia hilo.

OCD imepelekea maisha yangu ya kijamii kuwa magumu kwa kuogopa kufanya vitu kadhaa nikiogopa matukio mabaya kutokea. Mawazo ndiyo yametawala maisha yangu, nimekuwa mtu wa peke yangu peke yangu tu. Nashindwa hata kuwaeleza watu wangu wa karibu hali ninayopitia kwasababu nahisi hawatanielewa kwa kuona siyo tatizo.

Mbaya zaidi tatizo hili siyo rahisi kuondoka ni hali ambayo inanibidi niishi nayo. Ningependa kujua wale wanaopitia hali hii kipi kimewasaidia kupunguza hili tatizo.
Pole sana mkuu, napitia changamoto kama hii yani kwangu ni severe haswaa iko mixed na health anxiety disorder, naona watu wanakudhihaki hapa ila hawajui kua ni ugonjwa mbaya sana na ndo maana mara nyingi nashindwa hata kuwaeleza watu kwasababu wanaishia kudhihaki tu, nipo kwenye stage ambayo hata kutoka chumbani ni changamoto kila kitu naona kipo contaminated nje ya chumba, ningependa kujua umepata solution gani hadi sasa inaweza kunisaidia na mimi
 
Back
Top Bottom