Forgotten
JF-Expert Member
- Jul 20, 2018
- 3,518
- 10,839
- Thread starter
- #21
Hapo tiba ni therapy tu, nayo pia siyo 100% ila kama hali ni mbaya zaidi therapist ndiyo anaweza kukushauri kutumia anti-depressants.Pole sana mkuu, napitia changamoto kama hii yani kwangu ni severe haswaa iko mixed na health anxiety disorder, naona watu wanakudhihaki hapa ila hawajui kua ni ugonjwa mbaya sana na ndo maana mara nyingi nashindwa hata kuwaeleza watu kwasababu wanaishia kudhihaki tu, nipo kwenye stage ambayo hata kutoka chumbani ni changamoto kila kitu naona kipo contaminated nje ya chumba, ningependa kujua umepata solution gani hadi sasa inaweza kunisaidia na mimi
Yaani, unachopitia nakuelewa vizuri sana. Haupo peke yako, hapa JF na hata kwa jamii kwa ujumla bado hawana elimu kuhusu afya ya akili: ukimuelezea mtu shida unayopitia hawezi kukuelewa.
Jaribu kupitia community ya OCD kwenye Reddit, pia. Huko ndiyo huwa najifunza zaidi kupitia watu wenye changamoto hii.