Son of Gamba
JF-Expert Member
- Oct 26, 2012
- 4,720
- 6,957
Kwa wale wafuatiliaji wa Series maarufu ya THE 100 mtakuwa mnamfahamu yule muigizaji aliyejizolea umaarufu na kujulikana kwenye series hiyo kama the red queen akiigiza kwa jina la Octavia Blake, alikamatwa na Polisi huko Los Angels kwa kosa la kumpiga Boyfriend wake na kumsababishia maumivu makali.
Octavia ambaye jina lake halisi ni Marie Avgeropoulos alikamatwa baada ya Boyfriend wake kupiga simu polisi na kutoa taarifa kuwa amepigwa vibaya sana na baada ya polisi kufika na kujonea alama za kipigo zilizokuwa kwenye mwili wa jamaa huyo ilibidi wamkamate Octavia na kumpeleka Polisi.
Hata hivyo Boyfriend wake huyo alikwenda tena Polisi na kumwekea Octavia mdhamana na akaachiwa kwa bond ya dola elfu hamsini na kuwaambia Polisi kuwa yeye hakutaka wamkamate Octavia bali alichotaka ni kuokolewa kutokana na kichapo alichokuwa akipokea.
Katika Series ya THE 100, Octavia amecheza kama mwanamke jasiri, mpiganaji katili, asiyeogopa chochote kile kiasi anaogopeka sana kutokana na ukatili wake.
Hivi hapa kwetu kibongo bongo unaweza kupigwa na Girlfriend wako kisha bado ukaenda polisi kumwekea mdhamana??
Source; TMZ.