McLaren
JF-Expert Member
- Feb 19, 2025
- 1,170
- 3,743
Aliyekuwa mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Odero Charles Odero, amewataka viongozi wa kisiasa nchini kutumia kauli zinazojenga umoja, faraja na matumaini kwa wananchi, hususan katika kipindi ambacho taifa linapitia changamoto mbalimbali.
Akizungumza katika mkutano, Odero amesema Tanzania ipo katika wakati mgumu unaohitaji faraja, matumaini na kauli zinazowaunganisha wananchi badala ya kuwagawa. Amesisitiza kuwa viongozi wana wajibu mkubwa wa kuhakikisha maneno na misimamo yao yanasaidia kulinda mshikamano wa kitaifa ili kuepusha migawanyiko inayoweza kurudisha nyuma maendeleo ya nchi.
Odero ameeleza kuwa kauli za viongozi wa kisiasa zinapaswa kulenga kuleta watu pamoja na kusaidia taifa kusonga mbele, akionya kuwa mgawanyiko unaweza kudhoofisha mustakabali wa nchi. Ameongeza kuwa tukio la Oktoba 29, licha ya uzito wake, haliwezi kulimaliza taifa la Tanzania, akisisitiza kuwa nchi itaendelea kuwepo na kusonga mbele.
Aidha, Odero amewataka viongozi wa kisiasa kutotegemea mataifa ya nje kuzungumza au kuingilia masuala ya ndani ya nchi, akibainisha kuwa ni wajibu wa Watanzania wenyewe, hususan viongozi wao, kushiriki katika mazungumzo ya dhati kwa ajili ya kuliponya taifa