Odinga apanda daladala kwenda kazini

Odinga apanda daladala kwenda kazini

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
Odinga apanda daladala kwenda kazini.jpg

Muktasari:​

  • Kiongozi wa Azimio la Umoja nchini Kenya, Raila Odinga leo Jumatatu ametumia usafiri wa umma maarufu matatu au daladala kwenda kazini. Hatua hiyo imeibua mijadala mitandaoni.
Kenya. Kiongozi wa Azimio la Umoja nchini Kenya, Raila Odinga mapema leo Jumatatu, Julai 10, 2023 ametumia usafiri wa umma maarufu matatu nchini humo wakati akienda kazini.

Kabla na baada ya kupanda kwenye matatu, Odinga amesalimia na abiria wenzake na wengine wakionekana kumshangaa na kuzungumzana naye maneno mbalimbali.

"Nikiwa kwenye usafiri rahisi na rafiki wa umma nikielekea kazini asubuhi ya leo," ameandika Odinga.

Ndani ya usafiri huo uliokuwa ukipitia barabara ya Ngong-Nairobi, wapiga debe wakilalamikia gharama ya juu ya mafuta.

Abiria wengine walimweleza kuhusu gharama ya juu ya maisha, wakisema nchi haiendi kwenye mwelekeo sahihi.

Kiongozi huyo wa Azimio anaonekana kutilia maanani agizo lake la Juni 27, 2023 ambapo aliwataka Wakenya kuchukua hatua ili kuzuia Serikali kukusanya fedha zaidi kutokana na ongezeko la VAT kwa bidhaa za mafuta.

"Tumnyime (Rais William) Ruto ushuru wa mafuta kwa kuweka kikomo matumizi ya petrol na dizel. Njia moja ya kufanya hivyo ni pamoja na magari.

Tupange safari za mara kwa mara kwa gari moja kila inapowezekana; tutumie gari moja kusafiri kwa pamoja kila inapowezekana na kutembea badala ya kuendesha gari kila inapowezekana," alisema Odinga.

chanzo. Odinga apanda daladala kwenda kazini
 
Back
Top Bottom