Nakubaliana na wewe, kwangu mimi ni huko kuwafukuza watu au kushikana maungoni ndo tatizo langu lilipo. Haya ya kutokupokea rushwa nimpe hongera kwa hilo..!!
Video nashindwa kuipandisha hapa
Kwenye video wote walikuwa wameshikana wanaamuliwa na mlinzi
Lakini ukiangalia uandishi wa mleta mada inaokana alienda pale tayari akiwa na lake jambo(shari) nimesikia sauti ya mleta mada kwenye video akifoka time wanaamuliwa (anafoka huku anamfata mtumishi wa NIDA)
Odonyo nakushauri ungeongea na mtoa mada inbox. Na wewe pia ungejaribu kujitafakari kama kuna sehemu umekosea jirekebishe. Otherwise, kazi njema kama kweli wewe ni mtumishi muadirifu bro. Pamoja.
Mimi sio Odonyo ila binafsi namfahamu na ni mtani wangu kiukabila so namjua vizuri tu
Ukitaka kuona mleta mada ni mshari ni kuwa vitambulisho vya NIDA walitangaza watu waende wakachukue kwenye kata zao walizojiandikishia
Sasa mleta mada inaonekana alienda kukidai pale siku ambayo hakuna ratiba ya utoaji wa vitambulisho kwaiyo alitaka watu waache kazi zao wakamtafutie yeye kitambulisho chake