Mkandara... next time tutafanya kitu cha kweli hapa. Kwanza tutaanza na kidogo mwaka huu. Kabla hatujaweza kufanya kikubwa. Tutafanya kidogo kwa watu wa Detroit na kuona how we gonna handle it.. na kwa vile sisi tuna systems zetu wenyewe ni rahisi kusimamia mambo yenyewe.
Tatizo kubwa la Columbus ukiniuliza mimi ni kitu kimoja tu kikubwa, hawakukadiria wingi wa Watanzania watakaojitokeza kuitikia mwito wa kusherehekea pamoja. Hivyo, idadi ya waadaji ilikuwa ni ndogo sana in proportion to the number of people expected.
Nimewahi kuandaa tamasha kubwa la kimataifa pale Mwanza; Na hiyo ilikuwa hakuna mambo ya internet. Lakini tulijua kitu kimoja, ukiwaalika vijana kwenye shughuli ambayo inahusisha zaidi ya jambo moja you better be prepared kufanya mambo mengi kuwaridhisha. So tulikuwa na level karibu tatu katika kamati ya Maandalizi.
Tulikuwa na Timu Kuu (Watu sita) ya maandalizi niliyoiongoza ambayo ilisimamia kila kitu kuanzia ratiba, wageni mashuhuri, mialiko n.k, tulikuwa na timu ya chakula na vinywaji ambalo jukumu lao lilikuwa ni kuhakikisha kunakuwepo na chakula na vinywaji, tulikuwa na timu ya uhamasishaji (promotion), tulikuwa na timu ya Usalama na Ulinzi ambayo ili coordinate na jeshi la Polisi wilaya ya Mwanza mjini, tulikuwa na timu ya Usafiri na Malazi (ambao iliwahakikishia wageni wetu wa kimataifa hasa kutoka Uganda na Kenya kuwa watapokelewa na watapelekwa walikofikia n.k) n.k n.k
Siku ya tamasha walitokea watu karibu mia tatu hivi tukifanya shughuli zetu pale Gandhi Hall, karibu na Jengo la CCM. Matokeo yake ni kuwa maandalizi yetu yalikuwa yamezidi sana idadi ya watu kiasi kwamba watu waliondoka wakiwa si tu wameridhika lakini wamekosheka roho zao.
Katika lililotokea Columbus kutokana na uchache wa waandalizi hawakuweza kuadjust haraka baada ya kugundua kwa watu ni wengi kuliko matarajio yao. Ndio maana unapokwenda vitani wanasema hakuna mpango wa vita (war plan) ambayo inadumu mara baada ya kukutana na adui. Wangeweza kufanya quick adjustment na hata baada ya kukutana na washirika wao wengine waliojitokeza kuwaomba waingilie kati na kutoa msaada au kutoa support ya aina fulani.
All in all, walijaribu kuorganize kitu kikubwa sana ambacho kingekuwa cha kukumbukwa. Natumaini next time watakuwa wamejifunza kutokana na mapungufu yao. Hata hivyo, nawapa hongera kwa kujaribu kwani asiyejaribu hawezi kujua kama anaweza au afanye nini ili aweze next time. Hongera waandaji kwa jitihada zenu, na kufanikiwa kutukutanisha. Next time tunatumaini mtaweza kutuburudisha vya kutosha na kutufanya tusahau ya Columbus. Bado sijaondoa shilingi.