OFFICIAL : Samsung watoa simu yenye 7000mAh muda mfupi uliopita(M51)

reyzzap

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2014
Posts
6,813
Reaction score
21,807

Kwa mara ya kwanza Katika ulimwengu wa kampuni KUBWA na MAARUFU za Simu(Tuelewane hapo, usikimbilie ligi uje unitajie Doogee, Energizer au ulefone).

Hatimaye leo mchana samsung ametoa ingizo jipya katika series yake ya 'M', series inayojuulikana kwa kutoa simu zenye battery kubwa.
Hii ni Samsung M51 yenye ukubwa wa 7000mAh,huko German.

Ni mwezi haujapita ter 6 mwezi huu alitoa M31s yenye 6000mAh, na hapo nyuma alikua na M30s, M31 zote zikiwa na 6000mAh.

Ili kuokoa mda wanakupa fast charge ambayo itahitaji takribani saa moja na nusu kuijaza charge,
Ukiachana na Battery ambayo ndio inayoitambulisha hii simu zaidi, tukiangalia specs nyingine tunaona....

Camera 4 za nyuma, ikiwemo ya 64MP
Selfie ya 32MP

Processors ya pekee katika M-series maalumu kwa ajili ya gamingkutoka katika kampuni ya kimarekani Qualcomm Snapdragon 730G, katika mid range smartphone hii si haba.
High build quality wakitumia
Glastic(glass+plastic) katika rangi mbili nyeusi na nyeupe.
Display : full HD+ Super Amoled + infinity - O display.
RAM 6/8GB(market dependable)
Storage 128GB,

Kioo cha 6.67 inch
Face unlock na side fingerprint
Na specs nyingine nyingi..

Naomba ieleweke, hii ni MID range smartphone SI flagship, na kwa kujua kuna wapenda ligi humu pia ieleweke sijasifia simu, sijasema ni the best bali nimetaja specs zake, hasa hasa nikilenga battery..
Najua na Unajua kuna simu bora zaidi ya hii nyingi tuu.

Bei ni Tsh laki 9,
Ni Hayo tuu kwa wapenda simu zenye battery kubwa.
 
Sawa kongole kwao.....sisi wa mbagala tunaisubili ishuke maana iyo mia tisa si ni bei ya jumla maana huku itakuwa kwenye milioni na.......
 
Face unlock ya 2D nn? Maana ile tu inatosha huna haja ya FPS.
 
Asante kwa taarifa! Hiyo betri babalao!
 
Kwa hiyo betri chaji itakuwa inakaa hata angalau siku 2
processor ya sd730g inaweza kukaa zaidi ya Siku mbili kwa betri la mah7000 , kuna jamaa yangu alikuwa na ulephone ilikuwa inakaa Siku mbili kwa betri la 6000mah na processor ilikuwa ni Mediatek ya 14nm,
Sd 730g Ina 8nm Kama sikosei , lazima itakuwa very power effient
 
Inapatikana globally au India tu kama kawaida ya m series zote
 
Mkuu nataka kuagiza Doogee N20 ram 4, ROM 64, rear camera 16MP na front 8 kwa 218000/=

Na kuna ule phone ina specifications kama izo kwa 237000/=

Nipe neno Mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…