Officially nampitisha Harmonize kama msanii bora 2018

Officially nampitisha Harmonize kama msanii bora 2018

Kiukweli dogo anajitahidi sana na atafika mbali kwa jinsi anavyjituma....!
 
Harmonize namshauri atafute mgogoro na Diamond ikiwezekana aondoke WCB ili awe zaidi ya hapo.
Hawezi kuwa zaidi ya hapo akiondoka WCB jamaa anapewa attention kubwa na mondi kutoka na style yake ya kumfanya mondi ndie role model wake. Akiendelea kubaki WCB atakuwa zaidi ya hapo kwa kumtumia Dimond dogo atafika mbali sana.
 
siipendi WCB but hiyo haiwezi kuwa sabbu yakutompa harmo pongezi jamaa yuko vizuri mnoo naielewa sana DM chick naile ngoma aliyopewa collabo na Yule manzi wa kinyaruanda
 
Hana hata mtu wa kumsaidia kuhakiki lugha? WIMBO MKUBWA HALAFU , UNAKWENDA STUDIO, UNATAMKA " BENDELA" badala ya BENDERA halafu produzer anaona poa tuu mpaka anautoa hako kakosa cha kijinga kinachokera kwenye masikio ya wasikilizaji hakukiona? wakati anafanya edditing na mixing suala la lugha hakujua lina umuhimu?
"Mlingoti na Bendela"
"Anamwendo wa Malingo"
"Na kazuli shepu sula"

Jamaa nahisi ana tatizo la matumizi ya "R" na "L"
 
Anafanya vizuri sana ila diamond hakuna wa kumcompare nae[emoji23][emoji23]
 
"Mlingoti na Bendela"
"Anamwendo wa Malingo"
"Na kazuli shepu sula"

Jamaa nahisi ana tatizo la matumizi ya "R" na "L"
Hilo hatuwezi kumlaumu kuwa nano kwani ni asili alikozaliwa kukulia na kusomea. Lakini inapokuja kwenye suala la kuandaa program lazima uwe na wataalamu wa kuhakikisha ujinga kama huo haujitokezi. Uzuri kwenye recording za digital unaweza ku highlight kipande ulichokikosea na kukideleate na kuhakikisha unalazimisha matamshi ili kinaporuka hewani kisipate kukosolewa kwenye makosa ya kizembe " Negligent" Hapa wa kumlaumu sana ni aliye rekodi yeye aliona sawa hayo maneno mpaka anaadaa "master" kwake anaona sawa tuu???
 
Konde boy yupo vizuri sana, akikomaa zaidi atafika mbali. Wachache wanaomponda humu ndani wanatimiza tu ule msemo wa wahenga "Huwezi kupendwa na wote"
 
Hilo hatuwezi kumlaumu kuwa nano kwani ni asili alikozaliwa kukulia na kusomea. Lakini inapokuja kwenye suala la kuandaa program lazima uwe na wataalamu wa kuhakikisha ujinga kama huo haujitokezi. Uzuri kwenye recording za digital unaweza ku highlight kipande ulichokikosea na kukideleate na kuhakikisha unalazimisha matamshi ili kinaporuka hewani kisipate kukosolewa kwenye makosa ya kizembe " Negligent" Hapa wa kumlaumu sana ni aliye rekodi yeye aliona sawa hayo maneno mpaka anaadaa "master" kwake anaona sawa tuu???
Basi hilo kosa si la Harmonize pekee bali la Management yake yote plus Diamond, siamini kama Harmonize anaweza kutoa wimbo bila kumsikilizisha Diamond/managers
 
Kuna watu wataponda eti konde anamuiga bosi wake!!.. hao wawili wanafanana!.. ndo maana konde kaamua hata kupaka bleach ili tuu wapunguze mfanano!!... kwanza huu mwaka hakuna msanii mwenye kolabo nyingi kama konde boy... na tena kuna hii mpya sey shay ft konde boy... yaani jamaa ni 🔥
 
Jamaa nilimkubali kwa ile show aliyopiga kwao Mtwara. Ile performance aliifanya kwa hisia sana.
 
Kuna watu wataponda eti konde anamuiga bosi wake!!.. hao wawili wanafanana!.. ndo maana konde kaamua hata kupaka bleach ili tuu wapunguze mfanano!!... kwanza huu mwaka hakuna msanii mwenye kolabo nyingi kama konde boy... na tena kuna hii mpya sey shay ft konde boy... yaani jamaa ni [emoji91]
Fanya wainama wainuka....
 
Back
Top Bottom