Tetesi mpya zimeibuka katika ndoa ya mastaa wa muziki,
Offset na
Cardi B, baada ya
Offset kudai kuwa
Cardi B amemsaliti na hata kupata ujauzito wa mwanaume mwingine. Tukio hili limezua gumzo kubwa duniani, huku
Offset sasa akitaka mali kubwa kutoka kwa mkewe ili, kwa maneno yake,
"kuwalinda na kuwatunza watoto wao."
Kwa mujibu wa taarifa za
TMZ,
Offset amedai kuwa
Cardi B amekuwa akipuuza majukumu ya kifamilia kwa sababu ya uhusiano wa kimapenzi aliokuwa nao nje ya ndoa. Ameeleza wazi kuwa fedha ambazo zilipaswa kuelekezwa katika ustawi wa watoto wao zilitumika katika safari za kifahari na zawadi kwa mwanaume huyo anayedaiwa kuwa mpenzi wa Cardi.
Hali hiyo imemfanya
Offset, ambaye pia ni mzazi na msanii maarufu kutoka kundi la
Migos, kuwasilisha madai makali: anataka
Cardi B amuachie asilimia 70 ya mali zake zote, ambazo zinakadiriwa kufikia dola milioni 101. Aidha,
Offset anataka
Cardi B aondoke kwenye jumba lao la kifahari walilokuwa wakiishi pamoja, akisisitiza kuwa mali hizo zinapaswa kubaki mikononi mwake kwa ajili ya mustakabali wa watoto.
Kilichoibua mshangao kwa wengi ni kwamba hapo awali
Offset alikuwa akidai nusu ya mali (50%), lakini sasa ameongeza madai hayo hadi 70%. Kulingana naye, hatua hiyo ni kwa sababu anahisi amedhulumiwa mara mbili:
kwanza kwa usaliti, na pili kwa rasilimali za familia kutumika kwa mwanaume mwingine.
Mashabiki wa muziki duniani wamekuwa wakifuatilia sakata hili kwa karibu, huku wengine wakimuunga mkono
Offset na kuamini kuwa anatetea maslahi ya familia yake, na wengine wakimtetea
Cardi B wakidai kuwa madai hayo bado hayajathibitishwa kisheria.