John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,374
Kabla ya mchezo wa Yanga dhidi ya Biashara United uliopigwa Jumanne Februari 15, 2022 kwenye Uwanja wa Mkapa, kulitokea mvurugani baina ya ofisa wa Biashara United na wale aliowaita makomandoo wa Yanga.
Huyu hapa ofisa huyo anaelezea kilichotokea kabla ya mchezo huo wa Azam Sports Federation Cup kuanza.
“Mimi naitwa Alphat Juma, asubuhi ya leo (jana) baada ya kikao cha pre-match pale Uwanja wa Karume, Kamisaa akaturuhusu kwenda Uwanja wa Mkapa kukagua vyumba.
“Tulipofika tukakuta kuna dada wa JKT, akanionyesha vyumba viwili, nikachagua kimoja na kusaini kisha nikaingia ndani.
Wakati nakagua, wakaja security wamezaa sare zao nyekundu wakanilazimisha nifungue mlango, nilipofungua wakanivamia na kaunza kunipiga.
“Walikuwa wengi ikabidi nitoke, nilimjulisha Team Manager kwa njia ya simu na baadaye tukamjulisha Kamisaa wa mchezo ambaye alikuwa msibani.
“Nawajua na nimewakariri, hata sasa nikiwaona nawajua, ni watu wa Yanga, kuna mmoja wao wakati nakabana naye nilimsikia wanamuita Kondo.
“Alikuja hadi bosi wao wa JKT akasema hawa watu si wa Yanga kwa nini wanaingia vyumba vya Biashara? Nimeumizwa sana na walichokifanya.
“Tumesharipoti kote ikiwemo kwa TFF. Na kulikuwa na semina ya waamuzi hapa wameona kila kitu.”