Ofisa wa UM asema mapambano kati ya Ukraine na Russia yanaharibu utendaji wa uchumi wa Afrika

Ofisa wa UM asema mapambano kati ya Ukraine na Russia yanaharibu utendaji wa uchumi wa Afrika

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
Mjumbe wa Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP nchini Kenya Bw. Walid Badawi amesema, mapambano kati ya Ukraine na Russia yanaathiri vibaya utendaji wa uchumi wa Afrika.

Bw. Badawi amesema, mgogoro huo umesababisha ongezeko kubwa la gharama ya bidhaa za msingi barani humo.

Akiongea kwenye mkutano kando ya kongamano la ngazi ya juu kuhusu kuhamasisha uwekezaji wa malengo ya maendeleo endelevu ya Afrika, amesema kuwa nchi nyingi za Afrika zinanunua nafaka kutoka nje, na zinategemea kwa kiasi kikubwa mauzo ya ngano ya Russia na Ukraine. Sasa mnyororo huu wa thamani umeathiriwa na unaweza kuzidisha hali mbaya ya usalama wa chakula.

Ameongeza kuwa tangu mapambano kati ya Ukraine na Russia yatokee mwezi Februari, bei ya mafuta katika soko la kimataifa imeongezeka na kusababisha gharama kubwa ya matumizi ya nishati barani Afrika.
 
Bei imeongezeka kwa mataifa yasiojielewa. Wanaojielewa wana reserves na refinery plants wala huwezi sikia wakilia lia, Russia ina mafuta ghafi ya bei nafuu wajanja wanaagiza huko nyie bakini kulia lia. Ila si mliua Tipper makusudi sababu ya 10% pambaneni na hali zenu.

Tanzania bila kiongozi katili asiyependa ujinga mtabakia hivi hivi hadi mwaka 2100 utapofika. Viongozi wapuuzi watolewe kwa nguvu yeyote hata kwa jasho na damu.

Kiongozi ambaye anaona kuliletea taifa maendeleo ni option sababu analipiwa kila kitu na mshahara juu ni jipu ambalo linahitaji kuchomolewa na plaizi..
 
Russia imepatwa mafua dunia nzima inapiga chafya.

Wanatengeneza negative image ya warusi kwa Africa ili Urusi ilaanike lkn wapi?

Jinsi wazungu walivyokabili Covid-19 pamoja na vita ya Ukraine inaonesha hawa watu siyo smart kwa kiwango kilichodhaniwa na wengi.
 
Back
Top Bottom