Kuna wanaodai kuwa,ni bora sana MME NA MKE wakawa sehemu moja kazini wanasema faida ni nyingi tu. Na wengine wanadai hiyo haifai kabisa bora kuacha kazi kuliko kufanya kazi sehemu moja na mkeo/mmeo.TIJA ITAONGEZEKA AU ITASHUKA?(PRODUCTIVITY)mnasemaje jf?.Kuna jamaa hapa yeye na mkewe wote wahasibu,inaelekea walikutana chuoni.Mke alikuwa anafanya kazi mikoani(serikalini)sasa jamaa baada ya kuomba aletewe mkewe, wakuu wamemrejesha Dar lakini wamemweka ofisi moja section moja na mkewe,room moja.Jamaa kachanganyikiwa, anasema ofisi ziko nyingi tu mjini kwa nini wamempangia ofisini kwangu?au kunikomoa?........nilimuuliza tu kuwa kuna ubayagani kukitazama kutwa nzima kile ukipendacho?... sio siri...swali langu hakulipenda sana.