KERO Ofisi nyingi za umma, hususan masijala zinakabiliwa na tatizo la rushwa

KERO Ofisi nyingi za umma, hususan masijala zinakabiliwa na tatizo la rushwa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Kefaville

Member
Joined
Mar 21, 2013
Posts
93
Reaction score
11
Ofisi nyingi za umma, hususan masijala za wazi na za siri, zinakabiliwa na tatizo la rushwa. Kwa mfano, katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela, unapohitaji huduma inayohusisha faili lako, unaelekezwa kwenda masijala. Ukifika huko, unaambiwa kuwa faili lako halipo. Hata hivyo, unaambiwa kuwa ili lipatikane kwa haraka, unatakiwa kutoa fedha za “chai.”

Ukiamua kutotoa fedha hizo, faili lako linaweza lisipatikane kwa wakati, hali inayokunyima haki ya kupata huduma unayohitaji.

Inasikitisha kuona kuwa baadhi ya watumishi wa umma wanadaiwa kutumia nafasi zao kuwaomba wananchi fedha zisizo rasmi ili kuwapatia huduma ambazo wanapaswa kuzitoa kwa mujibu wa majukumu yao. Kauli kama “ongeza kitu kidogo ili upate huduma haraka” zinaibua maswali kuhusu uwajibikaji na uadilifu katika utoaji wa huduma za umma.

Je, mamlaka husika zinafahamu hali hii, na ni hatua gani zinazochukuliwa kuhakikisha wananchi wanapata huduma bila kulazimika kutoa rushwa?
 
Back
Top Bottom