Ofisi ya Ardhi inaweza kuzuia ujenzi?

Nino

Member
Joined
Jun 21, 2007
Posts
38
Reaction score
1
Habari?

Rafiki yangu, Mtanzania, amenunua ardhi kule Zanzibar kwa kufuata mashauri yote ya sheha wa kijiji, alipata kibali cha kujenga kutoka halmashauri lakini watu wa ofisi ya ardhi hawajafika kupima ardhi hii kwa sababu wilayani walimchelewesha sana. Alipopata kibali cha kujenga alianza kujenga. Sasa alipokwenda kwa Ofisi ya Ardhi aliambiwa kwamba amefanya kosa kubwa kuanza kujenga bila kibali chao. Wanadai kwamba kibali hicho si juu ya halmashauri.

Je, mnaweza kumsaidia kuelewa haki yake?


Asanteni sana.
 
Hiyo ni conflict of interest hapa hela zitamtoka sana mpaka kuweka mambo sawa ngoma itakuwa ni kabambe sana kwanza aliwezaje jenga nyumba bila ya kufanyiwa survey ya serikali (wizara ya ardhi)?alifanya makosa tangu mwanzo ni kama vile kujaribu kutembelea mikono badala ya miguu.Kazi anayo.M/Mpamba End.
 
Alianza kujenga kwa sababu alimwambia kwamba ya ardhi alitakiwa kupata kibali cha halmashauri tu! Na kwamba wizara inashughulikia vipimo na hatimiliki tu! Sasa makosa ni ya nani?

Asante sana.
 
Ndugu yangu watu ardhi wanamanyanyaso sana ki ukweli mi nimetoka jana tu kuulizia taratibu za upimaji na survey ya eneo Nimeshangaa gharama ni kubwa kuliko hata thamani ya eneo lenyewe.. Sijajua wanatumia vigezo vipi ambavyo ni sahihi. Kuhusu suala lako kiongozi ngoja wenye maarifa zaidi waje...
 
Ndugu Ambra mimi ninashangaa kwa sababu inaonekana kwamba Tanzania haina sheria zozote. Kila mtu ana sheria yake. Kila mtu wa serikali anasema utakiwa kufanya hivi na hivi... na kulipa kiasi hiki. Hata malipo yanategemea na mtu si na sheria. hayupo hata mtu mmoja anayekuambia anafuata sheria gani!
 
Ndugu Msherwampamba mimi na rafiki yangu hatujui kutembea na mikono. Tafadhali udondoe kipingele kipi cha sheria aliyovunja. Nakushukuru.
 
Kwa sheria ya zanzibar,Mtanganyika hana haki ya kumiliki ardhi kule. 2 issue ya building permit sio kazi ya watu wa ardhi pekee. Wasimamizi ni wahandisi na watu wa mipango miji,mtaalam wa ardhi anahusika kukagua umiliki tu
 
Hamna mtu anayeweza kutaja kipengele cha sheria ya ardhi? Hata hapa kila mmoja anasema yake bila kutaja sheria yenyewe na vipengele vyake!
 
Hamna mtu anayeweza kutaja kipengele cha sheria ya ardhi? Hata hapa kila mmoja anasema yake bila kutaja sheria yenyewe na vipengele vyake!

mkuu issue ya Zanzibar ni tofauti na bara. Ingekuwa bara huwezi kujenga bila kupata Building Permit na kimsingi kwa mujibu wa sheria unapewa Building Permit baada ya kuwa umepewa hati miliki ya kiwanja tajwa.Angalia kifungu cha 34 (2) cha sheria ya Ardhi no. 4 ya 1999. NB: Hii ni kwa bara tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…