Ileje
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 9,524
- 13,682
Rais Samia ana kila sababu ya kuivunja ofisi ya DPP na kuisuka upya kwa sababu imeshindwa kukidhi mahitaji ya Taifa na kuonyesha umahiri wake.
Itakumbukwa kuwa Mbowe alikamatwa yapata mwezi mmoja na nusu uliyopita na kuunganishwa katika kesi ya ugaidi inayowakabili watuhumiwa watatu waliokamatwa zaidi ya mwaka mmoja uliyopita. Katika kipindi chote hicho DPP alikuwa anapeleleza tuhuma hizi za ugaidi na akajiridhisha kuwa wana kesi ya kujibu.
Tofauti na mategemeo ya watu wengi inakuja kugundulika mahakamani mashtaka yamekosewa na hivyo kushauriwa kwenda kuyarekebisha upya. Haiingii akili DPP na timu yake nzima wamekaa mwaka mzima kuandika mashtaka yasiyokidhi viwango vya kuitwa mashtaka! DPP gani huyu anakaa na tuhuma mwaka mzima halafu anashindwa kuandika mashtaka? Kazi yake nini hasa kama hawezi kuandika mashtaka? Halafu mwaka mzima anaingia ofisini kumbe anakwenda kusoma magazeti na kunywa chai kwa gharama za kodi zetu!
DPP na timu yake nzima hawastahili kuendelea kukaa katika ofisi hizo za umma, watafutiwe kazi nyingine za kufanya au wastaafishwe kwa manufaa ya umma! DPP ameonyesha si tu uzembe bali hajui sheria wala taratibu za mahakama.
Ukosefu wa weledi wa DPP umeonekana duniani kote kwa sababu za umaarufu wa Mbowe. Je ni wangapi wasio maarufu wanasota mahabusu kwa sababu za ujinga wa DPP.
DPP hana sifa za kuendelea kuwepo ofisini atimuliwe mara moja!