Ofisi ya Kanumba "Kanumba the great Film" yafungwa rasmi!

Ofisi ya Kanumba "Kanumba the great Film" yafungwa rasmi!

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363


Stori:Waandishi Wetu

Inauma sana! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya kusikia habari hii kuwa ile ofisi ya aliyekuwa mwigizaji kinara wa sinema za Kibongo, Steven Charles Kanumba ‘Marehemu Kanumba The Great' iitwayo Kanumba The Great Films iliyokuwa maeneo ya Sinza-Mori jijini Dar imefungwa rasmi huku vitu vikihamishwa usiku.



Ofisi ya Kampuni ya Kanumba The Great Films illiyopo Sinza Mori Dar imefungwa rasmi huku vitu vikihamishwa usiku.

Tukio hilo la kusikitisha lililoshuhudiwa na wanahabari wetu lilijiri Februari 2, mwaka huu, majira ya saa 1:30 usiku baada ya kutonywa na jirani mmoja anayefanya biashara zake karibu na ofisi hiyo.
Shuhuda huyo alidai kwamba mtekelezaji wa zoezi hilo ni mmoja wa watoto wa Mama Kanumba, Flora Mtegoa (jina halikupatikana mara moja) ambaye aliamua kufanya shughuli hiyo usiku ili kukwepa kuonekana.


attachment.php


Marehemu Steven Kanumba akiwa na tuzo za filamu enzi za uhai wake.
"Ninyi Global mnapitwa, mtoto wa Mama Kanumba anahamisha vitu ofisini kwa Kanumba, tayari zoezi limeanza," alisema jirani huyo aliyeomba hifadhi ya jina na kuongeza kuwa ofisi hizo zinahamishwa mahali hapo kwa sababu kodi ya jengo hilo imeongezeka kutoka laki mbili za awali na kuwa laki sita kwa mwezi, gharama ambayo inatajwa kumshinda mama huyo.

attachment.php


Wakiendelea kupangua vitu.


Wanahabari wetu walifika eneo la tukio ndani ya dakika sifuri ambapo walishuhudia gari aina ya Toyota Canter likiwa limepaki nje ya ofisi hiyo huku watu wanaodaiwa kuwa ni wabeba mizigo wakiingia na kutoka ndani ya ofisi hiyo wakiwa na vitu mbalimbali kisha kuviingiza kwenye gari hilo.


Kwa ustadi mkubwa, mapaparazi wetu waliopiga kambi katika eneo hilo walishuhudia masanduku ya vioo yaliyokuwa yakitumika kuwekea CD na DVD za marehemu Kanumba yakipandishwa kwenye gari hilo.
Baada ya zoezi hilo kushika kasi, wanahabari wetu walizama ndani na kujionea hali halisi ambapo walishuhudia chumba kikiwa wazi huku picha za ukutani zikiwa zimeshushwa na kuwekwa pamoja na vitu vingine tayari kwa kupandisha kwenye gari.

...Akiwa kazini enzi za uhai wake.
Hata hivyo, mtu aliyetajwa kuwa mmoja wa watoto wa Mama Kanumba aliwazuia mapaparazi wetu kupiga picha za ndani ya chumba hicho na kujifungia mlango kwa ndani huku wakisitisha zoezi la kupakiza vitu kwenye gari kwa muda wakiwataka mapaparazi waondoke eneo hilo.
Akizungumza na gazeti hili, mmoja wa wabeba mizigo hao alisema kuwa, walifika eneo hilo na gari lao kwa ajili ya kuhamisha mizigo kutoka ndani ya ofisi hiyo na kuongeza kuwa yeye hakufahamu chochote zaidi ya mhusika mwenyewe ambaye ni mtoto wa Mama Kanumba.

Mama Kanumba alipopigiwa simu na mwandishi wetu alikiri kupandishwa kwa kodi ya ofisi hiyo kwa kiasi kikubwa na kudai kuwa alishindwa kulipa fedha hizo kwa kuwa hapati faida yoyote kutokana na ofisi hiyo zaidi ya hasara.


attachment.php

Gari likiwa maeneo ya Sinza Mori.
"Kwa kweli kodi imekuwa kubwa mno, siwezi kulipa maana tangu mwanangu afariki dunia (Aprili 7, 2012) siku hadi siku kodi imekuwa ikizidi.
"Kipindi Kanumba anafariki dunia kodi ilikuwa laki mbili kwa mwezi, tangu hapo imekuwa ikipanda mara kwa mara mpaka sasa ni laki sita kwa mwezi na wanataka nilipe yote ya mwaka mzima, kusema kweli nimeshindwa.
"Hakuna kikubwa ninachonufaika na kampuni kiasi cha kulipa fedha nyingi kiasi hicho japo nimefanikiwa kutoa filamu mbili tu mpaka sasa.
"Nimeamua kuachana nayo (ofisi) nitafakari sehemu nyingine ya kuendeleza kampuni," alisema Mama Kanumba.

Kufungwa kwa ofisi ya Kanumba kunakuja ikiwa ni siku chache baada ya kuibuka kwa skendo kuwa ilikuwa imegeuzwa kichaka cha ufuska na baadhi ya wasanii na machangudoa ambao usiku huonekana nje ya ofisi hiyo na wateja wao.
Hadi sasa haifahamiki kama ndiyo mwisho wa Kanumba The Great Films au itafunguliwa sehemu nyingine au ndiyo imekufa moja kwa moja japokuwa kuna taarifa kuwa mara baada ya ofisi ya Kanumba kufungwa, kwa sasa ofisi hiyo ina mpangaji mpya. Chanzo.GBP



 

Attachments

  • Gari likiwa maeneo ya Sinza Mori..jpg
    Gari likiwa maeneo ya Sinza Mori..jpg
    43.7 KB · Views: 1,882
  • Wakiendelea kupangua vitu..jpg
    Wakiendelea kupangua vitu..jpg
    33.6 KB · Views: 1,853
  • Steven.jpg
    Steven.jpg
    49.5 KB · Views: 1,883


Kuna msemo unasema asiyekuwepo na lake halipo. Wengi tunamkumbuka mwigizaji marehemu kanumba alivyobadili mchezo wa bongo movies mpaka kuwa ni tasnia yenye kukimbiliwa na wengi. Sasa habari tulizozipata ni kuwa ile ofisi yake aliyoiacha baada ya kufariki dunia, mama Kanumba na wadogo zake waliohidi kuiendeleza wameshindwa na wameamua kuifunga baada ya kukosa kodi ya kulipia jengo.

Mama Kanumba amekaririwa akisema kwa sasa kodi ni laki sita hela ambayo wameshindwa kuilipa kwani Kanumba aliacha kodi ilikuwa laki mbili.

Toka Kanumba afariki, ofisi hiyo iliweza kutoa filamu mbili tu na ambazo hazikufanya vizuri sana katika soko.
 
Sasa mlitarajia nini kutoka kwa mama yule ambaye hana weledi wowote katika tasnia ya filamu? Tatizo letu huwa tunadhani yoyote anaweza kufanya lolote wakati wowote kumbe haipo hivyo, aliloliweza Kanumba si lazima mama yake pia aliweze, Mama alilazimishwa kuogelea kwenye bahari asiyoifahamu! sasa eti ndani ya wakati wote tokea Kanumba afariki wametoa filamu MBILI tu na hazijaleta matokeo chanya, aisee!?
 
Haihitaji kuwa profesa wa uchumi ili kujua kuwa soko la filamu Tanzania limeyumba na hakika wanapumulia mashine, wapo ICU! Ila kuna kitu kinanitatiza! Mbona kunako mitandao ya kijamii hawa masuperstaa wanatuaminisha kuwa kila kitu kipo sawa, na maisha yao yametawaliwa na kufuru za hatari hatari yaani bata kwa kwenda mbele? Hivi mapato na matumizi yao vinaendana kweli? Halafu hatusikii kama wana dili nyingine nje ya tasnia husika! wanaishi vipi mjini hapa? Aisee haya pia ni maajabu kama yale saba ya dunia!
 
Halafu si ilikuwa inasemekana mama ni muuguzi,nimeshangaa kusikia bado yuko dar badala ya kuwa kituoni kwake.

a devil is a liar mkuu,naona mama starehe za dar zilimzidia akaacha mpaka kazi yake ya uuguzi
 
Mama wa marehemu kakutana wadada wa mjini wanaojua kutumia fweeeza, mama chali..
 
Dah aisee wauze hati miliki kwa asilimia flani wapatage Franchise kuliko kuzima jina la jamaa.
 
Kampuni ya Kanumba ilikuwa lazima ife baada ya kifo chake, kwa sababu haikuwa na mradi mwingine zaidi ya kutengeneza filamu.
Na kwa bahati mbaya haikuwa na filamu zilizo mali yake ambazo waweza kusema inaweza kuendelea kuziuza hata atakapokufa.
Kingine kampuni yake haikuwa na msanii anayeng'ara inayommiliki zaidi ya yeye Kanumba tu. Ni kama ilivyo kampuni ya JB.
Mwisho mfumo wa biashara ya filamu nchini umechangia sana kutokea kwa hali hiyo, kwani filamu karibu zote ni mali za wasambazaji.
Sio ofisi tu, hata magari ya Kanumba yameshauzwa karibu yote na Mama Kanumba anaishi kwa kubangaiza tu.
Watu hapa JF tunasema biashara ya filamu imeshuka wakati wasambazaji wanazidi kuneemeka licha ya TRA kuanza kukusanya kodi kwenye filamu.
Mtitu aliyeanza juzi tu kusambaza filamu zake mwenyewe ameshakuwa na pesa kuliko hata za huyo Idris na nimesikia ameshaanza ujenzi wa ghorofa.
Ni biashara inayozidi kuwa ya neema kwa wasambazaji. Fikiria inapofikia msambazaji anamlipa mwenye filamu milioni 42 unadhani yeye anavuna ngapi?
Ova
 
Back
Top Bottom