Ojuolegbha
JF-Expert Member
- Sep 6, 2020
- 1,278
- 797
Ameyasema hayo Agosti 10, 2024 wakati akifanya mazungumzo na Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mahmoud Thabit Kombo pamoja na Viongozi alioambatana nao waliofika Ofisini kwake Vuga kwa lengo la kujitambulisha tokea kuteuliwa kwao hivi karibuni.
Mhe. Hemed amesema Tanzania imekuwa na ushirikiano mzuri na Mataifa mbalimbali duniani hivyo kuwepo kwa uongozi huo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kudumisha ushirikiano ili taifa lizidi kupiga hatua kimaendeleo kwa faida ya wananchi wote.
Makamu wa Pili wa Rais amesema kumekuwa na ongezeko kubwa la watalii wanaoingia nchini hii inaonesha wazi kazi nzuri inayofanywa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki hivyo ameutaka uongozi wa Wizara hiyo kutafuta mbinu mbadala za kuzidisha ushirikiano na mataifa mbalimbali ili kuendelea kuongezeka kwa watalii siku hadi siku.
Aidha, Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar ameutaka uongozi wa Wizara hiyo kuzungumza na wawekezaji kupitia nchi mbalimbali kuja kuekeza Tanzania hasa Zanzibar kwani zipo sehemu nyingi za kuja kuekeza hasa katika sekta ya utalii, mafuta na gesi asilia.
Naye, Waziri wa Mambo Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo amesema Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais na Wizara ya Mambo ya Nje wamekuwa wakifanya kazi kwa karibu na ushirikiano hasa katika masuala ya uwekezaji na ushirikiano wa kimataifa hivyo atahakikisha mashirikiano hayo yanaendelea kudumu ili kuleta ufanisi nzuri wa kazi kwa pande zote mbili za muungano.
Balozi Mahmoud amemuomba Mhe. Makamu wa Pili wa Rais kwa nafasi yake ya mtendaji mkuu wa shughuli za serikali kuendelea kufanya kazi kwa pamoja na ushirikiano katika kujadili mambo mbalimbali ili kukamilisha malengo ya serikali zote mbili ya kuwaletea maendeleo wananchi wake.