DOKEZO Responded Ofisi ya Mikwambe Kigamboni wanachelewesha huduma ya kuunganisha umeme makusudi

DOKEZO Responded Ofisi ya Mikwambe Kigamboni wanachelewesha huduma ya kuunganisha umeme makusudi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Napenda kuwashirikisha changamoto niliyokumbana nayo wakati wa kuomba huduma ya kuunganishiwa umeme katika ofisi za TANESCO Mikwambe, Kigamboni.

Kwa kifupi, ofisi hiyo ni mpya na ina mazingira mazuri, lakini huduma ya kuunganishiwa umeme kwa wateja inaonekana kucheleweshwa kwa muda mrefu. Nimekwishalipia huduma hiyo miezi kadhaa iliyopita kupitia ofisi ya Mikwambe, lakini kila ninapofuatilia naelekezwa sababu ambazo hazieleweki na ninaendelea kuzungushwa bila kupata huduma niliyolipia.

Kutokana na hali hii, nimeanza kupata wasiwasi kuwa huenda kuna ucheleweshaji usio wa lazima katika utoaji wa huduma kwa wananchi.

Naomba msaada wa kupaza sauti kuhusu suala hili ili liwafikie wahusika na hatua stahiki zichukuliwe. Huduma bora kwa wananchi ni haki ya msingi, na watumishi wa umma wanapaswa kuwajibika katika kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu na kwa wakati.

WALICHOJIBU TANESCO 👇🏽
 
Habari, ndugu mteja.

Kwanza, tunaomba radhi kwa kuchelewa kukurejea. Tulikuwa na changamoto kwenye akaunti yetu, lakini kwa sasa ipo sawa.

Kutokana na muda uliopita, iwapo bado hujapata huduma, tunaomba ututumie namba yako ya maombi ya umeme ili tuweze kufanya ufuatiliaji na kubaini chanzo cha changamoto kwa lengo la kukusaidia zaidi.

Asante. ^CM
 
Back
Top Bottom