GE2025 Ofisi ya Msajili wa Hazina yatoa Wito kwa Wananchi kujitokeza kupiga Kura Oktoba 29

GE2025 Ofisi ya Msajili wa Hazina yatoa Wito kwa Wananchi kujitokeza kupiga Kura Oktoba 29

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
459
Reaction score
644
Ofisi ya Msajili wa Hazina imetoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura ifikapo Oktoba 29, 2025, katika Uchaguzi Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akizungumza kwa niaba ya Msajili wa Hazina, Nehemia Mchechu, Mkurugenzi wa Usimamizi wa Mashirika ya Kibiashara, Lightness Mauki, amesema kuwa kushiriki uchaguzi ni wajibu wa kiraia unaojenga demokrasia, umoja na uthabiti wa Taifa.

Mauki amebainisha kuwa kupiga kura ni chombo muhimu cha mabadiliko chanya, kinachowawezesha wananchi kuchagua viongozi wenye maono, uadilifu na uwajibikaji.

Aidha, amesema ushiriki mkubwa wa watumishi wa umma katika uchaguzi unaonesha mfano wa uzalendo, nidhamu ya kitaifa na uelewa wa majukumu yao ya kikatiba.

Ameongeza kuwa Ofisi ya Msajili wa Hazina inaamini kuwa ushiriki wa wingi wa watumishi wa umma katika uchaguzi huo utasaidia kuunga mkono juhudi za serikali katika kuimarisha utawala bora, kukuza uchumi endelevu na kuboresha ustawi wa wananchi.

“Kwa mantiki hiyo, Ofisi inatoa wito kwa wakuu wa taasisi na mashirika ya umma kuhakikisha watumishi wao wanapatiwa fursa ya kutekeleza haki hii muhimu bila kuathiri majukumu yao ya kikazi, kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi,” amesema Mauki.

 
Back
Top Bottom