SAUTIYANGU
New Member
- Oct 23, 2024
- 4
- 2
Ofisi ya msimamizi wa Uchaguzi kata ya Sogea Mjini Tunduma imefungwa kwa muda usiojulikana katika kipindi hiki cha Uchukuaji na urejeshaji wa Fomu za wagombea huku chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)kikilalamikia kunyimwa nakala ya Fomu walizorejesha kwaajili ya uteuzi wa wagombea.
Wakizungumzia changamoto hiyo viongozi wa CHADEMA pamoja na wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Serikali za mitaa katika kata hiyo wamedai mnamo tarehe 26 Mwezi huu walichukua na kurejesha fomu lakini walipoanza kufuatilia nakala ya Fomu waliyotakiwa kupewa kwa Mujibu wa Utaratibu kila wanapofuatilia wanakuta ofisi hiyo imefungwa.
Kwa upande wake Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Tunduma Bi Mariam Chaurembo ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya Mji Tunduma amekiri kuwepo kwa Changamoto hiyo na kuwasihi wanachadema kuwa warulivu wakati wanashughulikia changamoto hiyo kwani fomu zao zimepokelewa na kufungiwa katika chumba ambacho hawawezi kuzichambua kwa sasa mpaka itakapofika hatua ya Uteuzi.