GE2025 Ofisi ya Mufti Zanzibar yaeleza kutofunga Madrassa kipindi cha uchaguzi ili kuondoa hofu ya kutokuwepo amani

GE2025 Ofisi ya Mufti Zanzibar yaeleza kutofunga Madrassa kipindi cha uchaguzi ili kuondoa hofu ya kutokuwepo amani

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Ofisi ya Mufti Zanzibar, imeeleza sababu za kutofunga madrasa wakati wa kuelekea uchaguzi mkuu ili kuondosha hofu na kujenga taharuki kwa wananchi kwamba hakuna amani

Pia, imewatahadharisha waandishi wa habari kuzingatia weledi na kuacha kuandika habari zitakazoleta taharuki na kusababisha mgawanyiko miongoni mwa wananchi

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo Jumapili Oktoba 26, 2025, Katibu Mtendaji Ofisi ya Mufti, Sheikh Khalid Ali Mfaume amesema hawakuona sababu ya kufunga madrasa Oktoba 29, 2025 siku ya uchaguzi kwa sababu kufanya hivyo ni kuleta wasiwasi na taharuki kwa wananchi

"Hatukufunga kwa sababu bado kuna amani, sasa tukifunga madrasa kwa sababu ya uchaguzi tunaongeza taharuki na kuonesha kana kwamba hakuna amani, bado tuna amani hali ni shwari," amesema katibu mtendaji huyo.

Sheikh Mfaume amesema kuna taarifa potofu zinazushwa mitandaoni baada ya taarifa kutolewa za kufungwa kwa shule

1761478284220.png
 
Kwani zanzibar kuna tension gani wakati siasa za enzi ya CUF ile ya maalim seif hazipo? kule kuna SUKI waendelee tu kula urojo na uroda wao kwa amani huku wakikarisha watoto maandishi ya kiarabu
 
Zanzibar inaongozwa kiislam? Mbona huyo mufti ana nguvu sana kuliko wa bara?
 
Back
Top Bottom