DOKEZO Ofisi ya Rais Utumishi, TAMISEMI na Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga okoeni mtumishi huyu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mshauri,aende Utumishi HQ,au TAMISEMI-Dodoma.
 
Km mkurugenzi hataki kutoa barua aende kwa katibu tawala wilaya au mkoa na aeleze kuwa mkurugenzi hataki kutoa maelezo. Lakini pia nimetoa njia zingine za kisheria
Hizo Mamlaka Kama zina uwezo huo basi hii njia ni rahisi sana. Maana jamaa anataka barua yenye Uamuzi wowote ule ili hata kama ni kuchukua hatua za ziada basi aanzie hapo.
 
KWANZA AENDE AKASOME AL-BADEER HUKU AKISEMA HIVI "KAMA ANAONEWA NA KUDHULUMIWA WANAOMDHULUMU WAPATE HUKUMU KALI YA MUNGU NA KAMA HAONEWI WASIDHURIKE".HAKUNA NAMNA.
 
Hii hali ilimkuta kaka yangu. Alikuwa ni mtumishi H/W ya Kilosa, kada ya Ualimu, alienda kujiendeleza 2016 wakati huo akiwa na Diploma, kilichomkuta mpaka leo anajuta. Kadhia zao zinafanana 100% ila yy amekuwa kwenda kulima baada ya kugundua anapoteza muda. Hii n true story
 
KWANZA AENDE AKASOME AL-BADEER HUKU AKISEMA HIVI "KAMA ANAONEWA NA KUDHULUMIWA WANAOMDHULUMU WAPATE HUKUMU KALI YA MUNGU NA KAMA HAONEWI WASIDHURIKE".HAKUNA NAMNA.
Duh! Hii kali japo iko sawasawa
 
Serikalini watu wana roho mbaya sana hususani maafisa utumishi, Huwa wanafanya ofisi kama mali zao binafsi, mm ukiniharibia ofsn nakutafuta mtaani, Bora tukose wote, pili, nafasi za uteuzi kama wakurugenzi wa halmashauri, wakuu wa wilaya na ma das, hawana msaada Kwa watumishi na serikali Kwa ujumla kimsingi ni mizigo
 
Sasa si akafungue kesi mahakamani.
 
Watu wana roho mbaya jamani yaani mtu anafurahia mwenzake kukaa mtaani.na jalada akaficha sjui ndio kulipoteza roho mbaya hii.ndio maana wengine wanakutwagwa na mabalaa sababu ya roho mbaya
Watu wana roho mbaya,jamaa inaonekana anapitia kipindi kigumu sana,
Kama anawafahamu wazee watata wa huko bora awafuate alipe kisasi kwa namna yoyote,vinginevyo hilo jambo litaathiri sana future ya familia yake
 
Inaonesha kuna misuguano ya ndani kwa ndani.

Aende mahakamani, serikali kesi zote za wafanyakazi huwa inashindwa
 


My country Men, ubaya uliozidi vipimo
 
Tumeona nyaraka kwenda kwa RC/RAS ambazo nazo hazikuzaa matunda. Hiyo ya DSO/RSO, DC na TAKUKURU ni ushauri mzuri. Kwa ujumla tunakusanya maoni ili tukianza kuchukua hatua tusambaze taarifa kotekote ndio maana tunapaza sauti. Asante sana Boss
Aende kwa katibu mkuu utumishi, nimeona clip mitandaoni Arusha , Makonda anamsaidia mama mmoja alikuwa na tatizo kama hili akaenda kwa katibu mkuu utumishi, alifika mpaka ikulu. Wiki hii analipwa hela yake huko Arusha.
 
Aende kwa katibu mkuu utumishi, nimeona clip mitandaoni Arusha , Makonda anamsaidia mama mmoja alikuwa na tatizo kama hili akaenda kwa katibu mkuu utumishi, alifika mpaka ikulu. Wiki hii analipwa hela yake huko Arusha.
Asante sana kwa mchango wako wa kiutu kabisa.
 
Mtu anayefukuzwa kazi serikalini ujue amevumiliwa Kwa zaidi ya miaka hata miwili.

Hadi utinuliwe serikalini.... Umehojiwa sana na umetetewa sana lakini hubebeki.

Huyo huenda aliitwa kuja kuhakikiwa akazingua kwenda au alienda masomoni na kuunga mkataba private sector huko akajiona mjanja.

Watumishi wa serikali ukiwa na kosa unapaswa uwe mpole, Waite Kila mtu mkuu, boss, afisa na jitoe ufaham hata ulie. Mapema tu unasamehewa.

Uwapo kazini usitombe Dem wa boss Wala kumzoea, usiwe mshauri wa utawala, pokea mikoba ya wakubwa na muda wote wasifie viongozi wako kuwa wao ndiyo wameweka tasisi yenu kwenye mafanikio ya Sasa.

Utasitaafu Kwa amani.
 
Rudia kusoma bandiko letu hapo juu. Soma kwa kutulia. Tatizo lilianza walipozuia na kumtoa kwenye malipo ya mshahara bila kufuata taratibu. Walipomhoji na kujiridhisha na kubaini ukweli imekuwa vigumu kumrudishia haki zake. Bahati mbaya barua aliyonayo ni moja tu ya kuitwa kwenye kamati ya Maadili 2021. Na kwa utaratibu ilitakiwa Mwajiri awe ametoa maamuzi yake kulingana na findings za kamati!
 
Chama Cha Walimu hakijatoa msaada?
 
Natafuta sheria inayosimamia hivi vyama vya wafanyakazi hasa inasemaje kuhusu makato na namna ya kujitoa
Hakuna sheria inayombana mtumishi wa umma kuwa mwanachama wa chama cho chote cha wafanyakazi, kinachofanywa na viongozi wa vyama hivyo ni kuwasajili haraka pale watumishi wanapoajiriwa wakiwa bado hawajui kitu kuhusu utumishi na pia wakiwa bado na mawenge ya kupata ajira.

Lakini pia viongozi wa vyama vya wafanyakazi huchukua check number za watumishi wapya na kuzipeleka uhasibu, kwa hiyo mtumishi anaanza kukatwa ada ya kila mwezi kabla hajajiunga na chama chenyewe. Watumishi wapya wakati wote wanaogopa kuhoji kwa kuhofia ajira zao au vitisho vya viongozi.

Kwa hiyo kujiondoa ni kuandika barua kwa mwajiri wako na kusimamia utekelezaji wa barua yako uhasibu. Waajiri wengi hawavipendi hivi vyama vya wafanyakazi hivyo hufurahi sana watumishi wanapojitoa.

Sasa hivi waalimu wameanza kujitoa katika chama cha CWT na wengine wanajiunga na chama kipya kilichoanzishwa hivi karibuni.
 
Wakishindwa kukusaidia, Kuna utaratibu wa kudai Cha kwako?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…