vamda
JF-Expert Member
- Aug 1, 2012
- 895
- 571
Ndugu wana JF. Ofisi ya tigo (kontena) iliyopo mji wa KAHAMA tokea tarehe 20 hadi 22 novemba, 2013 imeshindwa kuwahudumia wateja wake eti kwa sababu hawana jenereta kwa ajili ya kuwasha kompyuta zilizoko hapo ofisini kutokana na kukatika umeme wa gridi ya taifa kwa muda wa siku 3 kama ilivyotajwa hapo juu. Inashangaza kuona ofisi ya kampuni kubwa kama hiyo haina hata jenereta KAHAMA. Pia mhudumu mkuu wa kiume wa hapo ofisini mara nyingi huondoka na kuiacha ofisi ikiwa na wafanyakzi ambao hawana ujuzi wa kutatua shida mbalimbali za wateja maana hutoa majibu kwamba muhusika ametoka. Ndiyo maana tigo KAHAMA watu wengi wanaiogopa kama ukoma...!!!!