Ili kufikia azma ya kupanua wigo wa utendaji wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali na kuongeza ukaribu katika kuhudumia wananchi, Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali ina Ofisi 17 ambazo zimefunguliwa kwenye mikoa yote yenye masjala za Mahakama Kuu ikiwemo Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na kwenye mikoa ya Dodoma; Mtwara; Iringa; Ruvuma; Tanga; Kilimanjaro; Arusha; Kigoma; Mara; Mwanza; Kagera; Shinyanga; Tabora; Rukwa; Mbeya; na Morogoro.
Dkt. Boniphace Luhende, Naibu Wakili Mkuu wa Serikali
Bora hata hizo ofisi zote zingefungwa tu Hali ya utoaji haki imezidi kuwa mbaya kuliko wakati mwingine wowote kwa Sasa mtu mwenye uwezo anaweza kukutengenezea kesi yoyote hata ya mauaji na huna pa kwenda mlundikano wa mahabusu kwa kesi za uonevu tu ni hatari kubwa utoaji dhamana kwa kesi hata zile ndogo ni shida kubwa rushwa imetamalaki kiasi cha kutisha Polisi Mahakamani na Magereza hivyo Hawa wote waondoke tu Jaji Mkuu amefeli Mwanasheria Mkuu wa Serikali amefeli DPP amefeli Waziri wa Mambo ya Ndani amefeli na system nzima imefeli.