Ofisi ya Waziri Mkuu ina Mawaziri Wawili na Manaibu kadhaa, hawa wameshindwa kumsaidia PM hadi kaongezwa Naibu Waziri Mkuu?

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Kimuundo Ofisi ya Waziri Mkuu imesheheni Mawaziri wa kutosha yupo PM mwenyewe, Ndalichako na Mhagama wakisaidiwa na Mawaziri wadogo akina Katambi.

Sasa sijaielewa kama Nishati itakuwa chini ya PM au Naibu Waziri mkuu atakuwa Nishati.

Kuna wakati Hayati Mkapa aliombwa na CCM amfanye Magufuli awe Naibu Waziri mkuu ili apambane na Matumizi mabaya ya fedha za Umma kwenye Wizara zote Lakini mzee wa Lupaso alisita.

Ngoja nijifunze zaidi Kwanini Biteko na Siyo Prof. Kabudi au Lukuvi?

Mungu wa mbinguni awabariki sana.
 
Hata mzazi unaweza kujitahidi kumfanyia kila unaloona ni wajibu wako kwake but no appreciation.

Ni kama inaundwa timu maalum.

Mungu ilinde Nchi yetu na Watu wake wote.
 
Kiufupi Majaliwa ameMbiwa kuwa uwezo wako mdogo na ujiandae kisaikolojia….ndani ya miaka mitano Biteko atakuwa waziri mkuu!
Sioni kama ana cha kupoteza kwa kuletewa huyo msaidizi.
 
Biteko ni tambala lililoonekana linaweza kutumika kwa faida ya mkalia kiti 'full stop ! Nothing more relevant is expected to yield with positive impact unless someone in the office surrenders to quit it for safety grounds, this is a blindly calculated strategy which eventuality is remorseful regret'.
 
Pia tuliambiwa Lukuvi na Kabudi ni wasimamizi wa mawaziri
 
Upo sahihi sn ni matumizi mabaya tu ya fedha za umma
 
πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘πŸ‘
 
Hivi list ya wazito kabisa hapo kwa PM si inatisha jamani? Au waTZ tumefikia milioni 100 kiasi tunahitaji ofisi ya PM ijazwe hadi imwagike?
 
Rais ana makamu, Mawaziri Wana manaibu ,Kwa nini Waziri Mkuu asiwe na Naibu?

Mwisho hao ni Mawaziri wa Wizara zilizo ofisi ya Waziri mkuu,PM ni mratibu wa Shughuli zote zote za Serikali
 
Si kodi zetu zinatapanywa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…