Ofisi za mamlaka ya mapato Tanzania (TRA ) kuwa wazi tarehe 30 NA 31 December, 2023

Ofisi za mamlaka ya mapato Tanzania (TRA ) kuwa wazi tarehe 30 NA 31 December, 2023

JF Kampuni Zote Zilizokuja Hapa KwaAjili Ya Huduma Ya Elimu Kwa Umma
Tanesco Ndiyo Niliona Walikuwa Active Na Wanajari Muda Bila Kuangalia Wameulizwa Swali, Ngani Ama Ushauri Gani Wananchi Wangependa Iwe

TRA Ni Nafasi Yenu Sasa Toeni Ufafanuzi Wowote Mtakaoulizwa Bila Jazba
Kumbukeni Hapa Kuna Watu Wote Wanaijua Hata Yale Msiyoyajua Ninyi
 
Mkuu nashauri mamlaka iwe pia inatoa matumizi ya nchi mzima kama inavyotoa mapato ya nchi nzima
 
JF Kampuni Zote Zilizokuja Hapa KwaAjili Ya Huduma Ya Elimu Kwa Umma
Tanesco Ndiyo Niliona Walikuwa Active Na Wanajari Muda Bila Kuangalia Wameulizwa Swali, Ngani Ama Ushauri Gani Wananchi Wangependa Iwe

TRA Ni Nafasi Yenu Sasa Toeni Ufafanuzi Wowote Mtakaoulizwa Bila Jazba
Kumbukeni Hapa Kuna Watu Wote Wanaijua Hata

Asante sana tumechukua kwa uzito mkubwa sana ushauri wako na kukuhakikishia tutafanya kama ulivyopendekeza.
 
Kuna biashara nimeianzisha..process za kupata lesen ni kama zimebadilika...nikaona isiwe tabu nikalipia machine ya EFD...cash taslim 580,000 sawa hapa nikaambiwa nitakuwa refunded kutokana na estimations nilizofanyiwa..:sasa nafata machine week ya pil hii naambiwa mpaka lesen nikawaambia ndio nipo kwenye mchakato...hapa kama sio mfumo wa halmashaur kubadilika ningekuwa nishamalizana nao...kuna mahusiano gan katika hili kama kuna baadhi ya zile mashine kubwa waliniambia niwalipe afu watahitaji tin number tuu...kuna kipato nakikosa na kuna kipato kinapotea kwa serikali...ufafanuz kidogo tuu
 
Ni kweli huu utaratibu wa kurejeshewa mashine ya EFD ya kwanza upo.Unachotakiwa uandike barua kwetu kwenda Mkoa ambao unalipia au utalipia kodi ili uweze rejeshewa kwa mtindo wa kutolipa kodi kufidia.Tunakushauri pia kwa kuwa kesho pia tupo wazi unaweza fika Mkoa wa Kodi husika na kuonana na Maofisa wetu wakusaidie na pia wapo maofisa Elimu na Mawasiliano kila mkoa tukusaidie kukuhudumia.
 
Mimi nimetumiwa sms ya kudaiwa kodi, na kodi nilishalipa tangu mwanzo wa mwaka, ni kawaida huwa nalipa full mwaka mzima, kuna namba za simu wameziweka kwenye hiyo sms kwamba niwasiliane nazo kama kuna maelezo, hizo namba zinaonyesha zipo diverted na huko hazipatikani.
 
Kumekuwepo na changamoto kwenye mitandao ya simu kutumiwa na watu wasio wema kuwaibia wananchi.Iwapo utapata taarifa kuhusiana na kudaiwa kodi na ukiwa unawasiwasi na taarifa hiyo tafadhali wasiliana nasi kwa 0800780078, 0700750075, 0800110016 namba za bure au chati nasi kwa whatsapp 0744233333.Tafadhali utilise kodi kwenye akaunti ambayo siyo akaunti ya TRA
 
MAMA alitoa msamaha kwa wafanya biashara walio na madeni ya zaidi ya miaka 5, lakini wakienda TRA kwa ajili ya kuendeleza biashara zao waendelee kulipa kodi wanakutana na deni na wanatakiwa walipe tena, wakati huyu mtu alipotea miaka yote hiyo shauri ya kushindwa kulipa madeni. Sasa hamuoni kama mnakwenda kinyume na maelekezo ya MAMA?
 
Ofisi za TRA zitakuwa wazi siku yavtarehe 30 na 31 Desemba ,2023 ili kuweza kuwahudumia wananchi na walipa kodi
1. Mmefanya vyema kutoa taarifa kwa umma mapema.
Hongereni sana kwenu kwa Jambo hili.
Inaonyesha kwamba Mmeanza kubadilika pole pole, hamko "rigid" kama TANESCO ambao mara nyingi sana wamekuwa wakitoa taarifa kwa umma ya "Kukatwa au Mgawo wa Umeme" baada ya umeme wenyewe kukatwa na siyo kabla.
2. Lakini Nina Ombi Kuu Moja kwenu nyinyi TRA Kuhusiana na Notification ya Kupokea Malipo ya Kodi ya Majengo.
Kwenye Risit za Manunuzi ya Umeme wa LUKU hazionyeshi Mchanganuo wa Fedha kwa Ajili ya Malipo ya Kodi ya Majengo,
Tafadhalini sana shirikianeni na TANESCO ili kuweza kurekebisha Jambo hili. Kiasi cha Fedha kwa ajili ya Malipo ya Kodi ya Pango kinapaswa kuonekana kwenye mchanganuo wa fedha ulio kwenye risit ya ununuzi wa umeme wa LUKU ili kutuondolea dhana ya uwepo wa vitendo vya wizi kwenye suala hili.
Thanks.
 
Serikali haina pesa inabidi wakusanye kodi toka kwa wafanyabiashara
 
MAMA alitoa msamaha kwa wafanya biashara walio na madeni ya zaidi ya miaka 5, lakini wakienda TRA kwa ajili ya kuendeleza biashara zao waendelee kulipa kodi wanakutana na deni na wanatakiwa walipe tena, wakati huyu mtu alipotea miaka yote hiyo shauri ya kushindwa kulipa madeni. Sasa hamuoni kama mnakwenda kinyume na maelekezo ya MAMA?
Mbona kimya mjibuni.
 
Taarifa hii ikufkie ewe ambaye umekaa na kufikiri utaenda kukwepa kulipa kodi kwa sababu ulikuwa "Unashehereka'.😅

Safi sana TRA.
 
Mbona kimya mjibuni.
Watoe majibu, wana nchi wanalia wanataka kufunga tena biashara sababu ya madeni ya zamani, mtu alishindwa kulipa deni akafunga biashara akapotea, amepata matumaini ya kuanza upya kutokana na agizo la MAMA, kwamba madeni zaidi ya miaka 5 asamehewe aanze upya. Waziri mkuu nae akasema hivyo hivyo, lakini TRA wanaendelea kudai kwa kusema hawana taarifa rasmi.

Je? Agizo la Raisi na Waziri Mkuu linahitaji URASIMI gani TRA?
 
Back
Top Bottom