Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 1,096
- 4,948
Naomba niseme ukweli kwamba ukitembea vyuo vikubwa Duniani utabaini Ofisi za waalimu ( Tutorial/Dr/Prof) NI eneo ambalo mnaweza mkakaa nakufanya majadiliano mkiwa na facilities zote.
For the first time nimefika university of Dar es salaam kumwona rafiki yangu ambaye nilisoma naye Ila Kwa sasa ni mwajiriwa wa Chuo kikuu cha DSM. Niseme ukweli hata yeye nafsi ilimsuta kunikaribisha ofisini kwake lakini hakuwa na jinsi ikabidi anialike.
Mazingira niliyoyakuta pale yanatia huruma. Hata kama ndo mnasubiri serikali iwajengee Ofisi hapana Madaktari na Maprofesa badilikeni. Haiwezekani sehemu mnayokaa Kwa zaidi ya masaa nane Kwa iwe mbovu kiasi hicho, chumba kimoja kidogo mnajibana wawili au watatu... Mnatumia public toilet, hakuna TV, hakuna desktop, laptop zenyewe zimechoka. Bora nisingeyafahamu haya nikanyamaza lakini naamini nikiandika hapa ntawaamsha watu kwenda kuwatembelea waalimu wao na kuwapa zawadi za meza za kisasa, viti vya kisasa, TV NK.
Labda nimeover expect lakini prof anapaswa awe mtu anayejijali, anayepokea machapisho na kuaandaa machapisho, anayefanya consultation every time that means anapaswa kuwa na Ofisi ambayo inamsadia kutekeleza majukumu yake.
LABDA NITOE USHAURI
1. Pamoja na miundombinu finyu, chuo kila Prof awe na chumba chake chenye meza nzuri, milango mizuri, TV na desktop
2. Tengeni vyumba maalum ambapo watakaa wasaidizi wa Maprofesa. Kwa maana nyingine incase kuna mwanafunzi au MTU anakuwa na program mahususi na Prof basi awe na sehemu anapoweza kukaa na kufanya KAZI.
3. Wekeni bajeti ya chai angalau Kwa wazee na wasomi wetu hawa watulize ubongo na kuwaza mambo mazuri yakuishauri serikali.
4. Waunganisheni kwenye miradi ya serikali wakaome Ofisi na mandhari wanaoishi wahitimu wao.
5. Maprofesa na Madaktari mliotolewa jalalani please wasaidieni wenzenu kifikra waishi maisha ya KAZI yanayoendana na hadhi ya elimu waliyonayo.
6. Kwa kuwa serikali na Maprofesa wenzenu haitawatekelezea niliyoandika 1-5 basi tengeni bajeti mfanye maboresho ya Ofisi zenu kwani muda mwingi wa maisha yenu mnautumia chuoni na ofisini kuliko sehemu nyingine yoyote. Mkikosa Amani na Ofisi mnayokaa mtapata tatizo la kiafya ikiwemo afya ya akili. Kama ninyi niwaalimu wetu onyeshe uprofesa wenu kwenye mazingira yenu ya KAZI.
Hii nimeandika Kwa UDSM lakini naamini vyuo vingine hawa wasomi labda Wana Hali mbaya zaidi yakuishi mazingira Duni wakisubiri serikali na mwajiri afanye miujiza.
Rafiki yangu najua ujajua kwamba nimeumizwa na Ofisi zenu Ila tambua kubadilika kunaanza nawewe... Mnamiliki vipi maguorofa huku mkiishi kwenye Ofisi Duni? Maisha yako ya fahari unaweza unayatengeneza mwenyewe.
I'll be back kuona mmebadilika? Kabudi was right those days.