Ofisi za Maprofesa na Madaktari wa UDSM zinathibitisha namna Taifa lilivyofeli. Je, hata majumbani kwao wanaishi kwa dhiki hivi?

Ofisi za Maprofesa na Madaktari wa UDSM zinathibitisha namna Taifa lilivyofeli. Je, hata majumbani kwao wanaishi kwa dhiki hivi?

Ofisi za nyingi za serikali hazijawahi kuwa serious kimuonekano, unakumbuka picha ya Jiwe aliyopiga akiwa ofisini? Labda baadhi tu.

Hicho chuo si ndio alikuwa anakiongoza Mukandala, ambaye uchaguzi wa 2020 alisema ulikuwa wa haki, baada ya kufariki Magufuli akasema uchaguzi ulitawaliwa na wizi.

Hapo si ndio katoka mzee wa Jalalani? Ambaye aliyakana yote ya Katiba aliyokuwa anayapigania akiwa hapo?

Kitila Mkumbo, si alikuwa hapo akipigania demokrasia? Baada ya kuteuliwa akageuka kabisa, akaanza kuimba mapambio.

List ni ndefu sana...

Sasa hao ndio unategemea maajabu kutoka kwao? Ndio maana CCM wameshawasoma, wanawateua U-DC ili wakawe chawa wao.
 
Naomba niseme ukweli kwamba ukitembea vyuo vikubwa Duniani utabaini Ofisi za waalimu ( Tutorial/Dr/Prof) NI eneo ambalo mnaweza mkakaa nakufanya majadiliano mkiwa na facilities zote.

For the first time nimefika university of Dar es salaam kumwona rafiki yangu ambaye nilisoma naye Ila Kwa sasa ni mwajiriwa wa Chuo kikuu cha DSM. Niseme ukweli hata yeye nafsi ilimsuta kunikaribisha ofisini kwake lakini hakuwa na jinsi ikabidi anialike.

Mazingira niliyoyakuta pale yanatia huruma. Hata kama ndo mnasubiri serikali iwajengee Ofisi hapana Madaktari na Maprofesa badilikeni. Haiwezekani sehemu mnayokaa Kwa zaidi ya masaa nane Kwa iwe mbovu kiasi hicho, chumba kimoja kidogo mnajibana wawili au watatu... Mnatumia public toilet, hakuna TV, hakuna desktop, laptop zenyewe zimechoka. Bora nisingeyafahamu haya nikanyamaza lakini naamini nikiandika hapa ntawaamsha watu kwenda kuwatembelea waalimu wao na kuwapa zawadi za meza za kisasa, viti vya kisasa, TV NK.

Labda nimeover expect lakini prof anapaswa awe mtu anayejijali, anayepokea machapisho na kuaandaa machapisho, anayefanya consultation every time that means anapaswa kuwa na Ofisi ambayo inamsadia kutekeleza majukumu yake.

LABDA NITOE USHAURI
1. Pamoja na miundombinu finyu, chuo kila Prof awe na chumba chake chenye meza nzuri, milango mizuri, TV na desktop

2. Tengeni vyumba maalum ambapo watakaa wasaidizi wa Maprofesa. Kwa maana nyingine incase kuna mwanafunzi au MTU anakuwa na program mahususi na Prof basi awe na sehemu anapoweza kukaa na kufanya KAZI.

3. Wekeni bajeti ya chai angalau Kwa wazee na wasomi wetu hawa watulize ubongo na kuwaza mambo mazuri yakuishauri serikali.

4. Waunganisheni kwenye miradi ya serikali wakaome Ofisi na mandhari wanaoishi wahitimu wao.

5. Maprofesa na Madaktari mliotolewa jalalani please wasaidieni wenzenu kifikra waishi maisha ya KAZI yanayoendana na hadhi ya elimu waliyonayo.

6. Kwa kuwa serikali na Maprofesa wenzenu haitawatekelezea niliyoandika 1-5 basi tengeni bajeti mfanye maboresho ya Ofisi zenu kwani muda mwingi wa maisha yenu mnautumia chuoni na ofisini kuliko sehemu nyingine yoyote. Mkikosa Amani na Ofisi mnayokaa mtapata tatizo la kiafya ikiwemo afya ya akili. Kama ninyi niwaalimu wetu onyeshe uprofesa wenu kwenye mazingira yenu ya KAZI.

Hii nimeandika Kwa UDSM lakini naamini vyuo vingine hawa wasomi labda Wana Hali mbaya zaidi yakuishi mazingira Duni wakisubiri serikali na mwajiri afanye miujiza.

Rafiki yangu najua ujajua kwamba nimeumizwa na Ofisi zenu Ila tambua kubadilika kunaanza nawewe... Mnamiliki vipi maguorofa huku mkiishi kwenye Ofisi Duni? Maisha yako ya fahari unaweza unayatengeneza mwenyewe.

I'll be back kuona mmebadilika? Kabudi was right those days.
Unashangaa Prof kukosa Ofisi nzuri? Ngoja nikuongezee na hili pia
1. Pale udsm jengo la Utawala ingia kwenye hizo public toilet hazina maji. Unakunya then inabidi utoke nje ya choo kuchukua Maji kwenye jaba moja lililowekwa hapo. Hakuna hata ndoo unachota na kikombe hadi mzigo utembee. HII nomeifanya mwenyewe miezi mitatu iliyopita nlipofika hapo kumsalimia ndugu yangu
2. Wakuu wa idara Huko UDOM hawana hata Secretary wa kutype barua. Unamkuta Prof au dr. anahangaika kuandika Barua ya paragraph moja.
3. Vyuo havina lab za kufanya tafiti za maana hasa kwa level za masters na PhD. Wakati wenzetu hata Prof au Dr. Anaweza kuwa na lab iliyokamilika sisi hata lab za kushare hakuna. Ukisikia chuo cha Tanzania kinasema kina lab ujue ni chumba kilichowekwa computer zenye windows OS na office package.😂️😂️😂️
4. Chuo kumnunulia mwalimu computer ya kufanyia kazi ni anasa kubwa. Ukiona mwalimu ana Laptop nzuri ujue kanunua kwa hela yake.
5. Vikifanyika vikao vya walimu matatizo yanayoongelewa ni vyoo vichafu, madarasa mabovu n.k. Yaani ni pety issues hadi unashangaa hivi hapa kuna profesa au PHD holder.😅️😅️😅️😅️

.......
Elimu yetu ilizikwa Kabla haijaanza.
 
Hivi wewe umewahi kuingia ofisi za wakusanya ushuru huku wilayani, utadhani wao sio wakusanya ushuru hata pazia hawana.
Nilienda kituo cha polisi pale Morogoro mjini mwaka 2016 nikakuta wanahesabu hela walizokusanya barabarani kwa mkono. Bila mashine. 😂️😂️😂️😂️😂️😂️😂️. Ajabu zaidi meza waliokaa ilikua imeteguka mguu mmoja wameunga na kipande cha mbao.
 
... Mnamiliki vipi maguorofa huku mkiishi kwenye Ofisi Duni? Maisha yako ya fahari unaweza unayatengeneza mwenyewe.
Mpuuzi mmoja huyu. Kama wanamiliki maghorofa tatizo liko wapi? Maana yake wana kipato kinachokidhi.
 
Kwa Mazingira kama hayo uliyoyakuta ndiyo utegemee kabisa hapo Kuzalishwa Intellectuals wa kulisaidia Taifa letu Kimaendeleo?
Wacha Maprofesa waendelee kukaa kwenye mazingira mabaya ili akili iwakae vizuri hapo mpaka World Bank walete pesa za kukarabati vyoo. Wakati wao wananunua V8. Aisee.
NB:ukipita pale Utawala unakuta V8 zimepaki kama yard ya kuuza magari. Nyingine zinaoza tu.
 
Back
Top Bottom