NIDA Ilemela ina changamoto kubwa katika utoaji wa huduma.
Sisi wananchi tunaohitaji huduma kutoka kwao tunaona hawawajibiki ipasavyo. Kwa mfano, baadhi yetu tuliojiandikisha mwaka 2023 hadi leo hatujapatiwa vitambulisho vya taifa, hali inayotukosesha fursa ya kupata baadhi ya huduma muhimu.
Naiomba NIDA Makao Makuu ichukue hatua za haraka kushughulikia changamoto hii ili wananchi wapate huduma kwa wakati.