Kasomi
JF-Expert Member
- Sep 3, 2014
- 11,030
- 20,391
Dah inauma sana
Najua humu wapo wafanyakazi either hao wa NIDA sehemu husika au sehemu nyingine.
Pia humu kuna viongozi na bila shaka watapitia bandiko hili.
Leo nilicho shuhudia ofisi za NIDA mkoa wa Mbeya kwa Kweli wale wafanyakazi wanajiona kama wametoboa Maisha yaani wanatesa sana wateja, kwanza hawana lugha nzuri kwa wateja wanaona wametoboa Maisha.
Yaani watu wanavyo fukuzwa utafikiri wao ndio Miungu wa sasa. Sawa pengine ni eneo lao la kazi ila naomba kama wapo humu au mnafahamiana nao waambie nimesema wajirekebishe maisha bado hawajatoboa nao ni waajiriwa bado.
Leo nilikuwa eneo hilo la ofisi sawa ni Sheria kuwa na shati lenye Rangi nyeusi, sasa leo kuja jamaa alizuiliwa kuhudumiwa kisa hana baadhi ya viambatanisho ikabidi amuazimishe mtu shati lake ili apate huduma eti nalo ni kosa. Sawa ni kosa na kama ni kosa ni vyema kumuelekeza ila wao kuona hivyo wanawafukuza eti hatutaki kuwaona muje siku nyingine hapo unakuta Mtu ametika Tukuyu kuja kupata huduma Mbeya mjini unamfukuza kisa kusaidiwa shati eti aje siku nyingine hizo nauli anazo poteza mtamusaidia yaani mnajiona mmetoboa.
Mwingine Mtu wa watu hajasoma anajaribu kuulizia kwa Mtu walau apate maelekezo vyema eti mnamfokea huyo Mtu ambaye anamuelekeza eti yeye ndio anajua sana na kumtisha kumtoa akijifanya Mwalimu sasa kosa lake nini.
Kwa kweli NIDA mkoa wa Mbeya mjirekebishe nina mengi ya kusema ngoja hasira zishuke Maana hapa nina hasira na hao jamaa hasa wapo wanaume wawili na kabinti kamoja. Hakika mjirekebishe Msijione mumeyaweza Maisha.
Nitarudi kuwasema vizuri imeniuma sana.