A
Anonymous
Guest
Ofisi za NIDA ni changamoto kubwa kwa wananchi. Unapeleka maombi yako na yanakaa hata miezi mitatu bila kushughulikiwa. Ukifuatilia, unaambiwa hukukamilisha taarifa fulani, na kibaya zaidi unaweza kukuta nyaraka ulizowasilisha zimepotea na hazionekani kabisa. Hali hii hukulazimu kuanza mchakato upya bila sababu za msingi, na mara nyingi hakuna hata neno la kuomba radhi.
Kwa nini kusiwe na mfumo wa mrejesho wa moja kwa moja kupitia SMS unaomjulisha mwombaji kuwa ombi lake limekataliwa au kuna taarifa zinazohitajika kukamilishwa, na kumwelekeza kutembelea ofisi kwa maelekezo zaidi?
Pia, kwa nini NIDA isiige mifumo ya taasisi kama RITA na taasisi nyingine za umma ambazo zimerahisisha utoaji wa huduma kwa kutumia teknolojia? Wananchi tunazungushwa bila sababu za msingi, huku muda wetu ukiendelea kupotea. Inaonekana kana kwamba thamani ya muda wa wananchi haizingatiwi ipasavyo katika baadhi ya ofisi za umma.