Ofisi za Wakuu wa Wilaya na barua za wapitao mitaani kuomba misaada!

Ofisi za Wakuu wa Wilaya na barua za wapitao mitaani kuomba misaada!

Librarian 105

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2023
Posts
261
Reaction score
356
Maana nimekutana na hawa watu (nawe pia naamini umekutana nao) wanapita mitaani kuomba wasaidiwe matibabu au masuala mbalimbali ya kijamii. Tusiwajadili wale matapeli.

Mana leo nmekutana na mhitaji kweli alipata ajali ya gari. Anahitajika kurudiwa upasuaji wa mguu. Ukicheki gharama ni kama laki sita hivi.

Ameenda kwa mkuu wa wilaya kuomba msaada ila amepatiwa barua ya kuomba msaada kwa wapita njia na maofisini. Je, hii munaitafakari vipi wakuu?

Mkuu wa wilaya yupo sahihi au?
 
Mjini kila mtu ananamna yake ya kuishi wewe fanya yako hayo mengine achana nayo.
 
Kwa mantiki hiyo hata kuminywa demokrasia au madai ya katiba mpya ni fursa mkuu?
Ni fursa kwa wanasiasa japokua inaathiri wote bila ya kujali umehusika ktk maamuzi ama haujahusika. Kimsingi suala la demokrasia na katiba ni pana na nyeti kuliko la vibali vya ma Dc kwa waomba misaada!
 
Ni fursa kwa wanasiasa japokua inaathiri wote bila ya kujali umehusika ktk maamuzi ama haujahusika. Kimsingi suala la demokrasia na katiba ni pana na nyeti kuliko la vibali vya ma Dc kwa waomba misaada!
Kweli. Ila hoja yangu bado sijapata majibu. Najiuliza,kama ni fursa, ni fursa kwa nani?

Tuachane na hawa wanaozunguka na vikombe au wheelchair
 
Huwa nakerwa sana na utamaduni huu wa wagonjwa kugeuzwa ombaomba tena kupitia ofisi nyeti za Wakuu wa Wilaya. Zaidi nimetafakari kwa nini Wakuu hao wasitoe vibali kwa wagonjwa hao kutibiwa bure huko maospitalini badala ya kuwazungusha mitaani wakiomba. Hiyo 'bukubuku' wanayochangisha mitaani na maofisini, wengi haijawasaidia kwa muda muafaka, maana ni hiyohiyo wanaitegemea kwa chakula. Zaidi tutegemee mpango wa Bima ya Afya kwa wote iwe suluhu ya kukomesha jambo hili.
 
Back
Top Bottom