Ofisini kwetu wananifanya mimi kituko

Ofisini kwetu wananifanya mimi kituko

Rikodi kisirisiri kwenye simu yako utani wao mchafu wote wanaokutania kisha nenda kawaripoti kwa bosi wenu, nakuhakikishia hawatakutania tena..
Nilirekodi audio tu ngoja nirekodi na video nitume kwenye group la ofisini.
 
Usiwawaze kaka zaidi ungana nao na usiwachukulie serious sana. Ila kwenye kazi kuwa makini sana maana wanaweza kukutoa mbuzi wa kafara kwa ishu ambayo hujafanya na wala hauijui.

Utani sawa ila kwenye kazi nyooka Mkuu ijulikane hauna kona kona hata ukishirikishwa kona kona jifanye boya usijihusishe maana utaangushiwa jumba bovu.
 
Namtumbo tafuta mnyonge mmoja hapo ofisini mshushie kipigo kikali utani wote utaisha
 
Hiyo tabia kwa English wanaita Bullying. Wewe ni victim wa bullying wamekutarget wewe kwasababu ndie easy target.

Utani huwa ni mzuri kama upo katika misingi ya heshima mfano mtu akawa anakutania kukuita Mkurugenzi, au mtendaji, au mtaalamu, au Baba mwenye nyumba, etc.

Ila utani ambao unakuwa na ishara ya dharau ndani yake una maanisha kuwa hawa watu waliokuzunguka wamechagua kukushusha kwa makusudi na inawezekana unapokuwa haupo karibu wanakuwa wakikujadili kama kituko na kukuongelea kwa vitu vya madharau sana.

Kila mtu ana mapungufu sio vizuri kumfanya mtu mwingine ajisikie vibaya au ajione duni mbele ya wengine kisha ukaita utani.

Kama mleta uzi hapa ameleta hii mada ni kwasababu hiyo tabia ya utani wa kulazimisha na wa kumshusha unamnyima amani anapokuwa eneo la kazi na hii inaweza pelekea mtu hata kupunguza ufanisi wa kazi sababu ya dharau kutoka kwa wenzake.

Haya mambo yapo sehemu mbali mbali, mashuleni, vyuoni, makazini kama kwa mleta mada na hata mtaani.

Unapoona mtu hayupo comfortable na neno au kauli fulani uliyomtamkia na akaonyesha sura ya kukerwa then ni vema kuacha. Usimwite mtu kwa majina ambayo yataonyesha wazi kuwa hayamfurahishi. Unamwita mtu Mwala sababu ni mfupi, au kitambi kwasababu anatumbo kubwa, au unamwita mpingo, au cheusi mangala sababu ni mweusi sana, unamwita mtu Cheupe au zungu kwasababu ni mweupe wa ngozi. Si vema kufanya hizi kauli maana haijakaa sawa.

Mleta mada mimi sikujui wala sikufahamu ila naelewa unachopitia kwasababu nilishajifunza na kujua madhara yake. Na katika maisha huwa sipendi mimi niwe chanzo cha mwingine kukosa furaha ili mimi ndio iwe burudani kwangu. Na ningelikuwa hapo ofisini ningewakemea hao wenzako tena kwa macho makavu kabisa kuwaambia huo utani mwenzenu hapendi sio sawa, anaumia ila ninyi mnaona ni sehemu ya burudani. Mtu anapotaka heshima mtreat kwa heshima, kama anataka matani basi taniana nae.



Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Piga makofi na ngumi za uso hao wapuuz , acha kukaa kizembe , waambie mimi wa tarime muraa
 
Kuna muda nakaa chini natafakari na kujiuliza why me yaani kila napokuwepo lazima kutatokea kitu ambacho kitanifanya nikose raha.

Kuna ofisi nipo nimejishikiza hapa mjini ila staff wenzangu wamenifanya mimi kama kituko wananidhihaki kwa kigezo cha utani yaani kila niwapo ofisini uanzisha mada za kuniponda na kuniona mimi wakuja na toka nilivyowaambia nimetokea Namtumbo wameacha kuniita jina langu wananiita Namtumbo.

Juzi nilisahau chaja nyumbani nikawaomba chaji nichajie kwa makusudi kabisa wakanipa charger type c sasa mi nilikuwa sijui kama ni type c nikawa naforce kuchajia wakaanza kunicheka siku nzima topic ilikuwa ni mimi sijui type c.

Jana kuna mtu alivua viatu ofisini kiukweli miguu yake ilikuwa inatoa harufu wote wakanikomalia kuwa ni mimi ndio viatu vyangu vinanuka.

Leo wamekuja na topic kuwa mimi ni mkubwa sana inaonekana ujanani mwangu nilichezea pesa kwenye ulevi maana sura yangu imekaa kilevi levi so wamenitolea mfano kama mtu niliyekosa ramani ya maisha ilibidi nikae kimya mwishoni wanaanza kusema Namtumbo usikasirike huu ni utani tu.

Sasa kuna siku nitatoka home nimevuta nahisi ndio mwanzo wa mwisho wa staff wenzangu kunizoea kiboyaboya.
hiyo siyo ofisi, ni kijiwe cha madalali wa vyumba
 
Hiyo ni bullying.. na kuna jamaa mmoja extrovert ndio atakuwa na ushawishi wacontrol hao staff wengine wkutanie wewe
 
Siku zote nasema mazoea ndio mwanzo wa kuvunjiana heshima na yote inaanzia siku ya kwanza kujuana.
Ili uheshimike siku ya kwanza kujuana na watu ni lazima 1: Usiwe muongeaji sana wala kucheka hovyo.
2: Usianzishe utani kivyovyote.
3: Weka uso serious (uso wa mbuzi/beberu).
4: Ongea taratibu na kwa umakini bila kupepesa macho(keep eye contact).
5: Ongea kwa sauti ya juu yenye bass kiasi iliyojaa ukakamavu na kujiamini.
5: Fanya kazi iliyokupeleka ofisini kwa nguvu zote mengine achana nayo sababu hayakuhusu.
6: Mtu akileta utani siku ya kwanza malizana nae hapohapo kiutu uzima na umwambie asirudie tena. Hiyo itakeep distance na kuweka mipaka ya heshima milele kwani watakuwa wanakujua.

Baadhi ya watu ni natural kuwa na hizo sifa wengine na wengine ni natural kwao kutokuwa na hizo sifa, hivyo kama unaona huo utani unakushinda basi bila shaka unajaribu kuishi maisha fake ili kuridhisha wakuzungukao (watu wasiokuwa na hizo sifa) hivyo kupelekea kuteseka. Au mostly sababu watu wengine ni washenzi tu by nature.

Baada ya hapo utakata mazoea ya kipumbavu ya kudharirishana na kuvunjiana heshima na cha muhumi zaidi utakata unafiki addition ni utaogopeka hii kama ukiapply siku ya kwanza. Usiwasikilize people pleaser wanaokwambia uwachekee hao washenzi, huo sio utani ni dharau za wazi.
 
hiiii kwahiyo Namtumbo ndo umekuja kutusema na huku[emoji23]
 
Back
Top Bottom