Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yaani wamgeuze kichekesho aendelee kuumia moyoni ili mpuuzi mmoja afurahi? hahahh haya mambo hayatokuja kunitokea mimi. Hiyo michongo unayosema haipo wala haitotokea jamaa ataishia kudharauliwa tu hayo ndio malipo kama asiposimama kiume.Ni utani,unaonekana hujui kukasirika huna baya na mtu,sio rahis kutaniwa na watu wote, wape kicheko wenzako inawezekana kupitia wewe siku huisha vzuri,wewe ndio kiunganishi cha furaha, wewe ndio mtani wao, kaa nao vzuri michongo mingi itakuja kupitia wao pia
Point tupu mtoa mada pitia hapaHiyo tabia kwa English wanaita Bullying. Wewe ni victim wa bullying wamekutarget wewe kwasababu ndie easy target.
Utani huwa ni mzuri kama upo katika misingi ya heshima mfano mtu akawa anakutania kukuita Mkurugenzi, au mtendaji, au mtaalamu, au Baba mwenye nyumba, etc.
Ila utani ambao unakuwa na ishara ya dharau ndani yake una maanisha kuwa hawa watu waliokuzunguka wamechagua kukushusha kwa makusudi na inawezekana unapokuwa haupo karibu wanakuwa wakikujadili kama kituko na kukuongelea kwa vitu vya madharau sana.
Kila mtu ana mapungufu sio vizuri kumfanya mtu mwingine ajisikie vibaya au ajione duni mbele ya wengine kisha ukaita utani.
Kama mleta uzi hapa ameleta hii mada ni kwasababu hiyo tabia ya utani wa kulazimisha na wa kumshusha unamnyima amani anapokuwa eneo la kazi na hii inaweza pelekea mtu hata kupunguza ufanisi wa kazi sababu ya dharau kutoka kwa wenzake.
Haya mambo yapo sehemu mbali mbali, mashuleni, vyuoni, makazini kama kwa mleta mada na hata mtaani.
Unapoona mtu hayupo comfortable na neno au kauli fulani uliyomtamkia na akaonyesha sura ya kukerwa then ni vema kuacha. Usimwite mtu kwa majina ambayo yataonyesha wazi kuwa hayamfurahishi. Unamwita mtu Mwala sababu ni mfupi, au kitambi kwasababu anatumbo kubwa, au unamwita mpingo, au cheusi mangala sababu ni mweusi sana, unamwita mtu Cheupe au zungu kwasababu ni mweupe wa ngozi. Si vema kufanya hizi kauli maana haijakaa sawa.
Mleta mada mimi sikujui wala sikufahamu ila naelewa unachopitia kwasababu nilishajifunza na kujua madhara yake. Na katika maisha huwa sipendi mimi niwe chanzo cha mwingine kukosa furaha ili mimi ndio iwe burudani kwangu. Na ningelikuwa hapo ofisini ningewakemea hao wenzako tena kwa macho makavu kabisa kuwaambia huo utani mwenzenu hapendi sio sawa, anaumia ila ninyi mnaona ni sehemu ya burudani. Mtu anapotaka heshima mtreat kwa heshima, kama anataka matani basi taniana nae.
Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app