Ogopa kutambulishwa watu wa aina hii

Ogopa kutambulishwa watu wa aina hii

matanga melly

Member
Joined
Jun 19, 2011
Posts
5
Reaction score
0
Kuna ofisa wa serikalai idara ya ukaguzi ofisi ya elimu wilaya ya babati,amekwishawaingiza watumishi wenzake na hasa walimu katika madeni makubwa kwani ukisha tambulishwa kwake atajifanya kuwa karibu sana na wewe na hata wakati mwingine kukutembelea nyumbani au mahali pa kazi kama mtu anayekjali sana.mie baada ya kuzoweana aliniomba nimkopeshe hela tsh/900000 ilikuwa ni mwezi wa tatu 2010 akadai kwamba mwezi wa nane 2010 atarudisha ,hadi leo june 2011 hajarudisha.nilipojaribu kumfuatilia amekuwa akitoa vitisho vya hapa na pale,wadau naombeni ushauri ukizingatia kwamba ni bosi wangu.
 
pole sana kwa mkasa huu mkuu...jitahidi tu kuongea na kibinadamu inawezekana anakuwa mkali kwa kuwa hana hela ya kukulipa..
pia karibu sana Jf,kuna jukwaa kwa ajili ya utambulisho.ukipita kule si vibaya mkuu.
 
Msamehe yote yaishe....na yataisha maana mtaanza tena kuongea vizuri!
 
Pole sana mjukuu, inauma sana na hivi hela imekuwa ngumu hivi. Hata elfu kumi unaweza ukaandamana. Ka mshtaki kwa wakuu na yeye.
 
Kama una evidence ya
Aina yeyote ile inayoonyesha
ulimkopesha basi nakushauri umshtaki.
 
kamuone dihenga amshughulikie, mishahara mitatu tu hela yako imeshatimia
 
kama una kithibitisho waweza kumshitaki au ndio yale mambo ya kukopeshana kirafiki bila evidence...........namna ya kumshitaki inakuwa ngumu...............pole sana

 
Back
Top Bottom