ha ha ha ha!pamoja na hilo mkuu pia kuna aina ya matukio hayaitaji presence ya Raisi hata kidogo otherwise tunakuwa too cheap.... mimi ningeunga mkono ningemwona mkulu anapokea msaada wa kuanzisha kiwanda cha hayo ma Yebo yebo (if not hizo tukutuku) bongo .... not kupokea maYeboYEBO bana
Ndiyo matunda ya uomba omba
Mwalimu aliwaomba Wachina hawa watujengee kwa mikopo nafuu kiwanda cha URAFIKI, UFI, reli ya TAZARA (tukaviua wenyewe!), misaada mikubwa ya kijeshi,.....JK yeye analetewa yeboyebo, pikipiki, wakati vitu hivi tayari vimejaa Kariakoo, mitaani!?
yaani wa TZ tumekwishilia mbali. jamaa anatoa promo heavy kwa Mil 51? just imagine hao wachina wakitumia hiyo picha kufanya promo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia Yeboyebo zilizotolewa msaada na balozi wa China nchini Tanzania Bwana Liu Xinsheng katika hafla fupi iliyofanyika ikulu jijini dar es Salaam jana asubuhi.Rais Kikwete alitangaza kuwa misaada hiyo itapelekwa kwa waathirika wa mafuriko wilayani kilosa,Mkoani Morogoro.
Kiwanda cha swala waliuziwa wahindi ambao wakakibadili kiwe cha kutengeneza tembe (dawa) kinaitwa shellys kipo pale mwenge. Hiyo ndo faida ya mwekezaji bana teh teh! utumbo mtupu nchi hii dah!"Baiskeli za Cheng shang kwa madaha ndio zenyewe zina nguvu imara kama simba. zinabeba mzigo zaidi ya punda."
Nimelikumbuka tangazo la baiskeli. Hivi kiwanda chetu cha baisikeli kipo? kinafanya kazi?
Akimpa waziri nafasi hiyo atakuwa anajipunguzia repyutesheni mbele ya jamii. Kwa taarifa yako ninategemea kufungua chekechea yangu kule kijijini na nitamualika mkulu aje na kumuhakikishia 100% coverage naamini atakuja tu!Brother MM, na kakako mwenyewe sometimes amezidi mno. Nafikiri wewe ni rafiki yake wa karibu, jaribu basi kumshauri ajaribu kudeligate baadhi ya mambo. Waziri anayeshughulikia maafa si yupo, kwanini asipokee yeye?
Mliambiwa mkanywe nae chai lakini ninyi mkafanya vinginevyo. Mtajiju sasaHuyu bwana hata hajui anafanya nini Ikulu, wakina Rostam walimburuza kumpeleka ikulu wakijua ufahamu wake ni mdogo sana ili wamtumie kwa manufaa yao, ona sasa anavyojizalilisha na kuidhalilisha nchi kwa ujumla. Hiyo hafla inaweza kuwa imeigharimu nchi zaidi ya thamani ya hiyo misaada ya kichina
...Muda si mrefu tutatumbukia shimoni pasi shaka. Wana TARIME wameanza tifu kama mbuzi wasio na mchungaji na subirini itaenea nchi nzima ndipo aliye shambani asikimbilie jikoni.mambo mengine ni aibu sana kwetu...tumekuwa kama vipofu tusio na mwongozaji