Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Sio kweli kwamba zinarudishwa dukani zina matumizi mengine na ni biashara kubwa inayowaweka watu mjini.. Nitakuja na ufafanuzi wa kinaHabari wadau!
Naomba kufahamishwa Kwa anayelijua hili, oil chafu na makopo ya oil yanayokusanywa na watu toka gereji za magari na pikpik zinaenda kutumia kwenye nini?
Nilipewa fununu kuwa kuna jinsi zinapikwa na kurudishwa tena dukani... Pia wanawasihi mafundi wakiwa wanafungua wafungue vizuri ili wasiharibu nembo wala kidumu cha oil.
Hii inakupelekea vyombo vyao Moto kuharibika sababu oil nyingi sasa hivi hazina ubora..., Kwan nilijaribu kumuhoji mmoja last week kuwa wanazipeleka wapi alikuwa mkali sn na hakutaka kunijibu. Wanapopeleka wengi ni eneo la kigogo mbuyuni opposite na shule ya msingi Lutihinda.
Kama ni kweli wahusika wa kudhibiti ubora wa bidhaa wapo wap?
View attachment 3119909View attachment 3119910View attachment 3119911View attachment 3119913
Tabata DampoWapi huko ?
Kigamboni
Buza
Temeke
Mbagala
Oil chafu( iliyokwisha tumika) ni biashara kubwa sana duniani na ina matumizi mengiDah! Kidogo moyo umetulia, jitahidi utuletee ufafanuzi ili tuendelee kua na amani.
1. Hutumika kama dawa ya mchwa kwenye mbao zile zinazoitwa 'treated'
2. Ikichanganywa pia na kemikali nyingine ni dawa nzuri ya vyoo vinavyotoa harufu..
3. Kupitia mchakato wa pyrolysis (Pyrolysis is the process of thermal decomposition of materials at elevated temperatures, often in an inert atmosphere without access to oxygen.)unapata mafuta yaitwayo I.D.O (Industrial Diesel Oil)
Matumizi yake
Kwa kawaida hutumiwa kama mafuta mbadala wa dizeli kwenye viwanda vya saruji, kioo, chuma, nk. kama nishati mbadala. Kwa kuongeza, inaweza pia kutumika kwenye majenereta ya mafuta mazito kuzalisha umeme. Kulingana na sifa za uchambuzi, mafuta ya pyrolysis hayawezi kutumika moja kwa moja kwenye gari. (Labda mpaka yachujwe tena kwa kemikali na kuongezewa viwatilifu sahihi)
Watengenezaji(wakandarasi) wanaojenga barabara pia hutumia sana IDO kwenye mitambo yso mikubwa na hata kwenye kuchemshia lami
Kinachoonekana mtaani ( wakusanyaji wenye madumu na baiskeli ni sehemu ndogo tu ya kaliba nzima ya Oil chafu
Kuna watu wana mikataba kabisa ya kununua oil chafu toka kwenye vituo vikubwa vinavyofanya service na makampuni makubwa ya magari