11 OUT of the 33 dead in Naivasha officers from the GSU Recce unit which protects President Kenyatta and VIPs, State House confirms.
Du!!!
Rais ameahirisha ziara yake katika Kaunti ya Narok ambapo alifaa kuzuru Jumanne Desemba 13 ili aweze kwenda kutembelea familia za maafisa 11 wa GSU wa kitengo cha kulinda watu mashuhuri waliofariki katika barabara ya Naivasha-Nakuru,” akasema msemaji wa Ikulu Manoah Esipisu.
Lori hilo lililokuwa limebeba bidhaa zinazoshika moto kwa urahisi na lenye nambari za usajili UAK 519C, liligonga tuta la barabarani na kisha kupoteza mwelekeo kabla ya kulipuka na kuteketeza magari mengine 12.
Kulingana na Mamlaka ya Usafirishaji na Usalama Barabarani (NTSA), magari 11 yaliyohusika katika ajali hiyo iliyotokea usiku wa kuamkia Jumapili yalikuwa ya kibinafsi huku jingine lilikuwa la usafiri wa umma.
Matatu ilikuwa imebeba abiria 14 ambao wote waliangamia katika ajali hiyo.
Lori hilo lilikuwa likitoka Mombasa na kuelekea Magharibi mwa Kenya.
Maafisa wa polisi wa Recce ambao ni tawi la kitengo cha GSU, walikuwa wakielekea jijini Nairobi wakitokea katika maeneo ya Bonde la Ufa ambapo Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto walikuwa walikamilisha ziara yao.
Gari lenye nambari za usajili GKB 961G, ambalo maafisa hao wa GSU walikuwa wameabiri liliteketea huku waliokuwemo wakiungua kiasi cha kutotambulika.
Akihutubia wanahabari katika Jumba la Harambee, Nairobi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Irungu Nyakera alisema kuwa bunduki tisa na risasi zilipatikana katika eneo la tukio.
Naibu wa Rais William Ruto alikuwa miongoni mwa viongozi waliozuru eneo la mkasa, Naivasha.
Waziri wa Usalama Joseph Nkaissery jana alisema kuwa serikali imeanzisha uchunguzi ili kubaini chanzo cha ajali hiyo huku akikanusha madai kwamba lori hilo lililosababisha ajali lilikuwa limebeba mafuta.
“Gari lililosababisha ajali lilikuwa lori dogo aina ya Canter lililokuwa limebeba bidhaa zenye uwezo wa kushika moto kwa haraka na wala si trela la petroli,” akasema Bw Nkaissery.
Waziri alisema kuwa serikali imeanzisha uchunguzi ili kubaini chanzo cha ajali hiyo.
“Hatima ya dereva wa lori hilo bado haijulikani. Tumeanzisha uchunguzi ili kubainisha ikiwa ajali hiyo ilisababishwa na matuta ya barabarani au utepetevu wa dereva wa lori,” akasema Waziri wa Usalama.
Add a comment