"kama mtu mwenye akili akikupa wazo la kijinga akijua na wewe una akili nawe ukalikubali (wazo hilo) atakudharau" - Nyerere (Mei Mosi 1995, Mbeya)[/QUOTE
Mzee Mwanakijiji,
Asante sana nilighafilika kidogo kwenye hiyo quote. Sasa kweli MAFISADI wanaonyesha kutudharau. Let's not let them get away with it this time. Naamini kabisa huyo MWEZA YOTE yuko pamoja nasi na hatatutupa.
Kuweni wa kweli sasa kwani saa ya mjaribu inakuja na imefika, siku ya Jumatano ijayo kama nilivyofanya mwaka jana nitaongoza sala ya "baraka na laana" na Mungu aliye mbinguni mwenye kutawala nyakati na nyakati, mmiliki wa nyota na sayari na muumbaji wa muda, kina, umbali na mwendo! na Mfadhili wa uhai wote atasikia.
Nasikia kuwa baada ya mzee Mandela kushika uongozi S/A kulionekana tatizo la usalama wa bahari yetu ya Hindi kuingiliwa hovyo bila serikali kugundua, hivyo Mzee Mandela akasema Watanzania mlinisaidia sana nami sipendi kuona usalama wenu ukiwa hatarini hivyo natoa mapesa muone mtayatumia jinsi gani kuimarisha ulinzi wenu pamoja na bahari yenu, mipesa hiyo ikaingia mikononi mwa BWM na watalaam wake wakupindisha mambo ndipo ikabuniwa Buhemba,Meremeta,Tangold,etc alimradi fujo ilianzia hapo kwani wote waliokuwa wanajua kuwa hii ni zawadi kutoka kwa Madiba walinufaika mpaka Buhemba ilipokufa, kitamu kingine katika ze comedy hii ni kwamba kwa maisha yote ya marehemu BUhemba mpaka ilipokufa na kuzikwa hakuna hata senti tano iliyoingia si Buhemba, serekalini, wala Nyumbu-TATC pale Kibaha. waliuza sana lakini pesa-0000....
Kwa hilo ndugu zanguni Pinda atasema nini zaidi ya kusema Meremeta ni siri ya serikali? (story hii ni habari niliyopewa na jamaa yangu aliyekuwa karibu nao katika kwapuakwapua)
We need a new government with a new Mandate.. turudi kwa wapiga kura. Let me look at the constitution...
Bibi Ntilie.. umesema maneno mazito na kimsingi umetupa ile ethos inayoongoza mjadala ndani ya CCM na serikali yake. Lakini huu mtindo wa kuitetea serikali yao ndio uliotufikisha kwenye matukio ya Februari. Wasipoangalia na Pinda naye anaweza kujikuta analazimishwa kujiuzulu kwa kulidanganya Bunge.
Haitakuwa mara ya kwanza duniani kwa waziri mkuu kulazimika kuondolewa madarakani muda si mrefu tangu aingie. Haiwezekani mtu atawale nchi kwa geresha na aongoze kwa hadaa. Ukweli utajulikana tu.
Katiba yetu ina vipengele vifuatavyo ambaavyo naamini vinaweza kutumika kutota katika hii time warp ya ufisadi. Pinda anakuwa kama Q wa Star Trek!
Katiba inasema kuwa Rais anaweza kulivunja Bunge endapo baadhi ya mambo yatatokea, miongoni mwa hayo ni:
Mimi naamini wabunge wakatae kupitisha mojawapo ya bajeti hizi zas serikali au hoja ya Waziri Mkuu ili hatimaye Rais alazimike kuvunja Bunge na turudi kwa wananchi na kuanza moja.
Kuhusu Majeshi yetu Katiba inasema hivi:
Sijaona mahali popote pale ambapo panampa madaraka Rais kuliamuru Jeshi letu lolote kufanya biashara ya aina yoyote isipokuwa iwe inahusiana na Vita na ulinzi wa nchi. NI lazima serikali ioneshe ni jinsi gani Meremeta na makampuni mengine yamehusishwa na masuala ya vita au ulinzi wa nchi. Yaani, hiyo vita iliyosababisha kuundwa kwa Meremeta na kuchotwa mabilioni ilikuwa inapiganwa wapi?
??????....
HahahahKikwete Yeye Hana Muda Na Tanzania, Keshokutwa Anaondoka Kwenda Zake Japan, Taarifa Za Ndani Zinasema Atapitia Na Dubai Kufanya Shopping Kidogo.